April 12, 2021

 


NAHODHA wa kikosi cha Yanga, Lamine Moro raia wa Ghana amesema kuwa ligi ya Tanzania ni ngumu kutokana na ushindani uliopo kwenye kila mechi ambayo amekuwa akicheza.

Lamine ni kinara wa utupiaji kwa mabeki wanaocheza ligi akiwa amefunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao.

Akizungumza na Saelhe Jembe, Lamine amesema kuwa tangu anafika Tanzania ameona namna ligi ilivyo kuwa ngumu kwa wapinzani kuonyesha ushindani mkubwa.

“Tangu nimefika Tanzania sijawahi kuona mechi rahisi kwangu hasa kwa Yanga, ushindani huo umekuwa ukitufanya nasi tuzidi kuongeza juhudi ili kupata matokeo,” .

Mchezo wao uliopita mbele ya  KMC, Yanga ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 baada ya dakika 90 kukamilika, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya kwanza ina pointi 51 na KMC ipo nafasi ya 6 na pointi zake ni 36.

1 COMMENTS:

  1. Ligi ya tz hususan round ya pili kila timu inakuwa na lengo la kusaka point ili iwe mazngra mazr ko timu kubwa chondechonde wasiingie na matokeo uwanjn.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic