BAADA ya mwendelezo wa sare kuwa mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga na kuwakatisha tamaa baadhi ya mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuhusu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kiungo wa timu hiyo, Haruna Niyonzima amebainisha namna ambavyo watachukua kombe hilo.
Niyonzima raia wa Rwanda, alisema anafahamu Wanayanga wengi wanaonekana kuvunjika moyo na kukata tamaa juu ya timu yao, lakini amesema njia pekee ambayo wataitumia kutwaa ubingwa msimu huu ni kutoruhusu kufungwa wala kutoka sare tena kwenye michezo iliyosalia.
Akizungumza na Spoti Xtra, Niyonzima alisema wao kama wachezaji wanajua nafasi ya kuchukua ubingwa bado wanayo kwa sababu timu ipo kileleni na watakachokifanya kwa sasa ni kushinda mfululizo bila kurudia makosa.
“Njia pekee ya sisi kutwaa ubingwa ni kujituma uwanjani kwa dakika zote 90 na kutorudia tena makosa ya kufungwa au kutoka sare, kinachotakiwa kwa sasa ni kushinda tu.
“Sisi kama wachezaji tumeshakubaliana katika hilo. Niombe tu mashabiki wetu kuwa pamoja na timu katika wakati huu mgumu.”
Kwenye msimamo wa ligi Yanga ipo nafasi ya kwanza ina pointi 54 baada ya kucheza mechi 25. Leo inakutana na Biashara United iliyo nafasi ya 12 na pointi 30 kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.
Kwani mechi mliyofungwa na mlizotoka sare mlikubaliana iwe hivyo?? Mnadanganya mashabiki wakati wenyewe mnajua ubingwa hamchukui
ReplyDelete