April 10, 2021

 


KIKOSI cha Yanga leo kimelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni David Bryson wa KMC alianza kupachika bao la kuongoza dk 28 kipindi cha Kwanza lilisawazishwa na Yacouba Sogne dk 46 kipindi cha pili. 

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba zama za Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo ulikamilika kwa ubao kusoma KMC 1-2 Yanga.


Ikiwa nyumbani KMC haikuwa na chaguo zaidi ya kuruhusu pointi tatu zake zikisepa mazima mbele ya Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji wa KMC, Charles Ilanfya atajilaumu mwenyewe kwa kuwa alikosa nafasi ya wazi kipindi cha Kwanza akiwa yeye na mlinda mlango Farouk Shikalo baada ya kupiga shuti ambalo lilikwenda nje kidogo ya lango.


16 COMMENTS:

  1. Ile yanga ya mwambusi mliyosema ni balaa ndo hiyo imetoa sare au ni nyingine

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo ni ile timu ya kaze, mrundi wa barcelona academy

      Delete
  2. Timu inayotaka kwenda CAF kwa nguvu zake yenyewe imetolewa kamasi na kmc kikosi cha laki 8

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wachezaji wa KMC walikuwa wakionekana kuwachezea faulo nyingi wachezaji wa Yanga.
      Nyinyi si mrudi mkutane nazo kama za Prison!

      Delete
    2. ndugu labda unadhani Yanga imeishamaliza kukutana na Prison..Je unatambua mechi ya robo fainali FA Cup , Yanga itacheza na Prison tena Nelson Mandela.hiyo ndiyo nafasi pekee iliyobaki ya Yanga kwenda kimataifa kwa jasho lso...kwani baada ya sare hii Yanga ina nafasi ndogo sana ya kuchukua ubingwa ligi kuu..ki uhalisia haipo.hivyo usiongee kama hujui uendapo..au unadhani tangu Prison walivyocheza na Simba sasa hivi wako dhaifu...Au Yanga wanaelewana na Prison kiasi kwamba hawatacheza kwa nguvu kama walivyocheza na Simba..yetu macho na masikio

      Delete
  3. Poleni sana mabingwa wa jadi. Safari ya toka suluhu ndio mnaianža upya na Mnyama mlimbeža jana mkitaka a hapse sabs

    ReplyDelete
  4. Wachovu hao tu,kila siku watakaa tunahujumiwa na tff wakati kila mtu ameona walivyopigwa pira spana na KMC,mwaka huu watafurumusha makocha mpaka wachoke wakati huo mnyama anaingia semi final

    ReplyDelete
  5. Sasa tutana nani wa kufukužwa na pia watapeleka mashtaka ya maonevu. Cha muhimu Senžo atatengeneža kila kwa baraka make tangu alopojiunga

    ReplyDelete
  6. Maskini Yanga mpaka wanatia huruma,kweli hujuma wanazolia kila cku ndiyo hizi sare za mfululizo? Naona kutimuliwa kwa Mwambusi kunanukia maana Cedrick akitimuliwa baada ya sare ya police

    ReplyDelete
  7. Wakashitaki tena wizarani

    ReplyDelete
  8. Sasa hao ndo utopolo kwenye ubora wake baada ya kusoma albadiri na kutamba gazetini

    ReplyDelete
  9. Mnawadanganya na vichwa vyenu vya habari pale hamna kitu

    ReplyDelete
  10. Madeni ya wanyonge wasioutaka kuwalipa, bila ya kuishukuru Simba na kusema watapita kwa jitihada žao wala si kwaajili ya Simba ndiko kunakowaumiža. Mchezaji au kocha hata akiwa na uwežo wa kupindukia akifika kwao anapoteža kila kitu na wanapenda shari na wameshakuwa maarufu kila pahala hapana wa kuwapa pole wakowapi kina Mwamnyata hawaonekani. Juu ya kuahidi wa bilion ža shilingi pia na kupigwa na burada pia haikusaidia

    ReplyDelete
  11. Mwambusa ni bonge la kocha na anaipenda sana Yanga lakini asitaraji kitu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic