April 27, 2021


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi leo Aprili 27 kimekwea pipa kuwafuata wapinzani wao Tanzania Prisons, Rukwa,Songea.

Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali na ikiwa itashinda inatinga hatua ya nusu fainali ikipoteza itakuwa haina nafasi ya kusonga mbele. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 30, Uwanja wa Nelson Mandela na mabingwa watetezi wa taji hilo ni watani zao wa jadi Simba.

Nahodha Msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa wana nafasi ya kupata ushindi kwenye mechi ambazo zimebaki na watapambana kufanya vizuri.

Msafara huo utaweka kambi kwa muda Mbeya kabla ya kuwafuata Tanzania Prisons , Sumbawanga.

6 COMMENTS:

  1. Hee mtihani mwengine huo kabla hatujapona jaraha la jana

    ReplyDelete
  2. Hivi mwandishi ni mhutu nini?Rukwa na Songea wapi na wapi?

    ReplyDelete
  3. Kama mwandishi hajui tofauti ya Rukwa na Songea ni kwa vipi atakuwa na weredi kwenye kazi yake?

    ReplyDelete
  4. Hivi hawa waandishi kwenye hii blog wanafanya makusudi au vilaza kweli maana ni hovyo kabisa yaani

    ReplyDelete
  5. Jamani Luna watu hawajui hiyo tofauti yaa mikoa, wala msishangae. Na hiyo habari ilisomwa na mtu zaidi ya mmoja, kabla ya kuchapishwa, na wote hawakuona hilo kosa. Ndio waandishi wetu walivyo..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic