YACOUBA Sogne, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Yanga leo amewanyanyua mashabiki wa timu hiyo baada ya kufunga bao la ushindi lililowapa pointi tatu mbele ya Biashara United.
Ikiwa inanolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwabusi ilikamilisha dakika 90 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United na kuwafanya wafikishe jumla ya pointi 54 wakiwa ni namba moja kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Katika mchezo wa leo Biashara United walikuwa imara katika kusaka jambo lao kipindi cha kwanza na walifanya moja ya jaribio kali kipindi cha kwanza ila mikono ya kipa Faroukh Shikalo iliweza kuokoa hatari hiyo.
Pia kipa namba moja wa Biashara United kipindi cha kwanza aliweza kuokoa michomo ya Carlos Carlinhos, Yacouba Sogne na Deus Kaseke jambo lililofanya mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza ubao kusoma Yanga 0-0 Biashara United.
Ni dakika ya 59 ambapo Yacouba alipachika bao hilo likiwa ni bao lake la sita kwenye ligi na kuwafanya Biashara United wasiwe na chaguo la kufanya kwa kuwa mpaka mwamuzi Emmanuel Mwandembwe anapuliza kipyenga ngoma ilikuwa Yanga 1-0 Biashara United.
Mgore pamoja na wachezaji wenzake watatu ikiwa ni pamoja na Ally Kombo walionyeshwa kadi za njano kwenye mchezo wa leo uliovuta hisia za mashabiki wengi.
Sasa tumefurahi kwani tumepata faraja na kurejesha lile lengo letu la kurejesha ubingwa na tu naamini hakuna wa kutuzuwia kwa hilo LA muhimu kwa sasa tudibadili kocha yumpe nafasi na kumuamini huyu Mwambusa jana watani walijiinamia kwa ushindi huo mkubwa. Yupo kileleni naamini hapana wa kutushusha tena
ReplyDeleteMhhhhhhh!!!!! Ushindi wa tia maji tia maji roho mkononi matumbo yanacheza dakika zote tisini
Delete