April 10, 2021

 


MABONDIA wa ngumi za kulipwa Halima Vunjabei na Zulfa Macho kila mmoja ametamba kumchakaza mwenzake leo Jumamapili katika pambano la Queen of the Ring ‘Malkia wa Ulingo’ ambalo litakuwa ni la ubingwa wa dunia wa UBO litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar.

 

Katika pambano hilo la ubingwa wa Dunia wa UBO kwa wanawake ambalo limeandaliwa na Peak Time Media na kudhaminiwa na Global Tv Online, Gazeti la Championi, Smart Gin, ITV, Radio One, Uhuru FM, Clouds Media, Benki ya CRDB na City Mall Gym huku kiingilio chake kikiwa ni Sh 10,000 kawaida na Sh 20,000 kwa VIP.

Mabondia hao wametambia jana mchana mara baada ya kupima uzitoka katika uwanja wa Ubungo Plaza kabla ya pambano hilo ambalo linatarajia kupigwa leo Jumapili katika ukumbi hio.

Wakizungumza mara baada ya kupima uzito mabondia hao wameonyesha uchu wa kutaka kulipiza kisasi kwa kila mmoja akimwambia mwenzake kuwa atachezea kichapo kikali leo ndani ya ulingo.

Zulfa Macho ambaye ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Yusuph Macho alisema kuwa alisema haitokuwa rahisi yeye kupigwa na Vunjabei kwa kuwa amerudi kwake ili kumfundisha adabu katika mchezo huo.

“Nakwambia wewe, nimerudi kwa ajili yako na hautoweza kunipiga kwa sababu nimekuja kukufundisha adabu kesho (leo) hautoweza kutoka nakwambia”, alisema Macho.

Kwa upande wa Vunjebei alisema kuwa hawezi kupigwa na mabondia wa kawaida na hataki kuongea sana kwa kuwa kazi yake itaonekana ulingoni.

“Sina muda wa kuongea sana ila ninachotaka kukukwambia tutakutana ulingoni na kazi yangu ndiyo utaijua kwa sababu najimini na hauna uwezo wa kunitisha,” alisema Vunjabei.

Mbali na wakali hao maabondia wengine ni waliopima uzoto na watapigana leo ni Mwanne Haji dhidi ya Sarafina Julius, Agnes Kayange dhidi ya Mwajuma Pengo, Grace Mwakamele dhidi ya Asha Gota wakati Salma Kihombwa dhidi ya Mariam Mungi, Zawadi Kutaka dhidi ya Martha Kimaro, Fatuma Yazidu dhidi ya Dorothea Muhoza na Leilah Yazidu dhidi ya Happy Daudi.

Kwa upande wa mabondia wa kiume ambao watasapoti kwa kupanda ulingoni kuzichapa ni Loren Japhet dhidi ya Hamisi Morinyo, Ismail Galiatano atacheza na Nassor Madimba, Charles Tondo atakwaana na Sunday Kiwale.

George Bonabucha atavaana na Chidi Mbishi, Beka Ustaz atacheza na Idrisa Juma, Fadhil Chamile atapambana na Ramadhan Idd, Ibrahim Kiboko atamkwaa Nasibu Habibu na Abdallah Luanja dhidi ya Gialunca Branco kutoka Italia.

Stori: Ibrahim Mussa na Hawa Aboubakar

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic