May 8, 2021


 MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga uliotarajiwa kuchezwa leo Mei 8 umeahirishwa.

Sababu kubwa ya mchezo wa leo kuahirishwa ni kutokana na mabadiliko ya muda wa awali ambao ulipangwa kuwa saa 11:00 jioni ila ghafla Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) likatuma taarifa ya kubadili muda mpaka saa 1:00 usiku.

Kwa mujibu wa Yanga wameeleza kuwa hawawezi kucheza mchezo huo kwa kuwa TFF imekiuka kanuni ya kubadili muda  kanuni ya 15, (10) za Ligi Kuu Bara ambayo inaeeleza kuwa;"Mabadiliko yoypte ya muda wa kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali,".

Yanga ilipeleka kikosi uwanjani saa 11: 00 na wachezaji walifanya warm up kisha Simba walifuata baadaye.

Kupitia ukurasa rasmi wa Simba wa Instagram waliandika namna hii:"Mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans umeahirishwa.

"kipekee tunawashukuru mashabiki wetu waliojitokeza Uwanja wa Mkapa kutushangilia,".

17 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Kughairishwa ndio Neno sahihi katokana na asilo ya neno lenyewe lilikochukuliwa na sio kuhairishwa

      Delete
  2. Aliyeahirisha mechi nani?TFF au Wizara?Kulikuwa na tukio la kitaifa muda wa mpira au?Isije kuwa kuna watu wameingia choo cha kike!

    ReplyDelete
  3. Eti kughairishwa. Fani ya uandishi imejaa makanjanja

    ReplyDelete
  4. The game was not postponed but boycotted by Young fc aka autopolo fc what a shame

    ReplyDelete
  5. Aibu, Aibu, Aibu TFF,wizara

    ReplyDelete
  6. Msiilaumu timu ya Yanga.Someni kanuni ya TFF kuhusu kama mechi itaahairishwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mechi ya yanga nq azam azam ilikuwa ichezwe saa 10 ikaairishwa hadi saa 2.15 na taarifa ilitolewa saa 8 mchana, mechi ya yanga na biashara ilikuwa ichezwe saa 10 ikasogezwa hadi saa 1 usiku na taarifa ilitolewa saa 8 mchana mbona yanga hawqkugoma

      Delete
  7. Inaumiza xana mashabiki hii kwann wasipange ratiba zao mapema ujinga huu

    ReplyDelete
  8. Heri lawama kuliko fedheha. Kama unajiamini unacheza mpira hakuna kulalama.

    ReplyDelete
  9. Mechi ya Yanga vs Azam ilibadilishwa kutoka saa 10 hadi saa 2:15 usiku na matangazo yalitolewa saa 6 mchana siku hiyohiyo ya mechi. Mechi ya Yanga vs Biashara United ilisogezwa mbele kutoka saa 10 hadi saa 1 na taarifa zilizotolewa saa 8 mchana siku hiyohiyo ya mechi. Katika mabadiliko hayo ya ratiba hatukuona watu wanagomea mchezo Je, ni kweli sababu za Yanga zina mashiko au kwasababu ya msukumo wa mganga wao ambaye aliandaa manyanga yake kwa ajili ya saa 11?
    😂😂😂
    Bongo Sihami Walaiiiiiiii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haya mazoea yanatakiwa yakome tuendeshe michezo kwa kanuni tulizojiwekea hii hali ya kutojali kanuni inavitesa Sana vilabu video go wamekuwa wakilalamika Sana juu ya ratiba hakuna anayesikiliza
      Mtani hapa nampa kongole yake

      Delete
    2. Maoni sahihi kabisa. Kwanini TFF wasizingatie kanuni na wskubaliwe wakati wote upuuzi wao?

      Delete
    3. Wewe usilinganishe game ya yanga na biashara au vinginevyo Kwanza kutofautisha kati ya yanga vs biashara au simba vs namungo tunapokuja kwenye suala la la Derby Lina umuhimu wake na Lina upekee wake ndio maana hata maandalizi yake huwa sio ya siku moja au tatu hiyo yote Ni kuonyeshana Ni nakna gani hii Derby huwa na upekee wake hivyo huwezi kuhairisha kuzembezembe tu pasipo sababu za kimsingi kwa mujibu wa kanuni ya TFF yanga imefanya jambo sahihi kwani kwa kuendelea kufumbia macho tabia hizi zitaendelea kuzolotesha soka letu,Ifikie wakati TFF wasimamie kanuni na sio kuendesha soka kimazoea.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic