May 8, 2021

 


BAADA ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga kughairishwa leo Mei, 8, uongozi wa timu hiyo umesema kuwa ulikuwa unajiamini na ulijiandaa kwa ajili ya mchezo wa leo.


Ni Yanga waliamua kuondoka uwanjani kutokana na ratiba ya muda kupelekwa mbele ghafla ambapo awali ilikuwa uchezwa saa 11:00 jioni na ukapelekwa mbele mpaka saa 1:00 usiku.


Didier Gomes,  Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa walijipanga kwa ajili ya mchezo wa leo ila wameshtushwa na kilichotokea kwa kuwa wote walipokea taarifa muda mmoja. 


"Hamna namna kwetu imekuwa ni mshtuko kwa kilichotokea, tulijandaa na tulikuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.


"Zaidi ni kwamba tunaweza kusema kwamba kwa mashabiki ambao walijitokeza kuona burudani haijawa hivyo tunarudi kambini kwa ajili ya maandalizi mengine kwani tunatarajia kuondoka Jumatatu,".

Kikosi cha Simba kiliwasili uwanjani nankupishana na wachezaji wa Yanga ambao waliingia uwanjani saa 10 na kufanya mazoezi kwa ajili ya kukiaanda kikosi chao na muda waliokuwa wanautambua ni ule wa saa 11:00. 


Simba inatarajiwa kukwea pipa Jumatatu kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs.

27 COMMENTS:

  1. Mmezoea kuburuzwa ndio maana klabu yenu ina CEO na General secretary

    ReplyDelete
  2. Sisi tunacheza mpira uwanjani majungu na kulalamika tumewaachia Utopolo. Mechi zenu dhidi ya Azam na Biashara zote zilisogezwa mbele siku ile ile ya mechi ba wala hamkususia. Leo ushirikina umewaponza mpaka mnakataa maagizo ya Serikali.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha uongo mechi na Azam kulikuwa na sababu maalumu ya matumizi ya Uwanja ulitumika kwa dini ya kiislamu

      Delete
  3. Ijapokuwa sheria ilivunjwa. Kwani ingelikuwa nini wangekubali kucheza au ndio kuonesha kuwa wana msimamo usiotetereka? Kilichotokea sasa ni kuvurugika kwa ratiba. ubishi usiokuwa na faida na huku Simba ikiwa na mchezo huko Africa Kusini tarehe 14 vipi ipangiwe mechi kabla ya hapo

    ReplyDelete
  4. Sheria,kanuni na taratibu hazipo kwa ajili ya kuwaadhibu wadogo,mara ngapi tff inafungia,kutoza faini na hata kufungia wadau kwa kukiuka taratibu,naamini kwa hili wote wajuudhuru.

    ReplyDelete
  5. Simba wasicheze hii mechi kama yanga walikubali mechi zao za azam na biashara kusogezwa mbele mbona hii wameikataa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siyo kweli mechi ya Yanga na Azam ilihairishwa kwakuwa uwanja ilikuwa utumike kwaajili ya dini ya uislamu Shughuli maalumu lakini hii ya simba hakuna sababu yoyote

      Delete
  6. hakuna sababu ya msingi ya Yanga kupeleka timu uwanjani saa kumi na mojakwani walijua Simba hawatakuwepo wala marefa hawatakuwepo.Je hakuna mechi nyingine ya Yanga ilishabadilishwa muda hadi saa moja na taarifa waliipata saa nane lalini wakakubaliana na matokeo hayo. kuahirishwa ni masaa 24....je muda kusogezwa mbele ni masaa 24...Yanga haijawahi kusogezewa muda mbele na bado wakacheza?kama ndiyo kwa nini leo wamegoma?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwahiyo mwizi akikamatwa akajitetea mbona nilishaiba huko nyuma sikukamatwa anaachiwa?

      Delete
    2. Punguza makasiliko ili ratiba ibadilike inapaswa vilabu husika vishiriki mjadala na vikubali pia
      Je hilo lilifanyika achana na 24 hrs au kupewa taarifa inatosha??
      Siku nyingine jielewe we ni namna thaman yako

      Delete
  7. Wamechungulia wakaona goli nane (8) zinawahusu wakaamua kukimbia. Utopolo bhana!

    ReplyDelete
  8. Yanga wapo sahihi "simba wapewe hizo point tatu"

    ReplyDelete
  9. Kwanza hatujaambiwa sababu yeye mashiko ya mechi kusogezwa mbele hasa

    ReplyDelete
  10. Hata Yanga wameshangazwa cse hii mechi ilitakiwa ichezwe toka Feb ,By KARIA and Co wanatuchezea akili Why?????

    ReplyDelete
  11. Point tatu Kamwomve Job Ndugai Dodoma atawapa

    ReplyDelete
  12. Mbona game ya simba na mtibwa ilikuwa ichezwe usiku but mida ya saa saba ama nane mchana ikarudishwa nyuma na kuchezwa saa kumi why simba haikupepesa wala mtibwa haikupinga gozi likarindima uwanjani wakala khamsa zao na hakukuwa na malalamiko yoyote.vp wazee wa sagamiko mgongo wazi uto fc wajitie kususia game?wana jambo lao babu yao wa moro walomtumia game ya 1_1 aliwatahadharisha kuwa leo kuna khamsa hadi thamaaniya toweni timu faster.mazuzu haya majinga kinyama.

    ReplyDelete
  13. Mazoea ya kuvunja taratibu tuliojipangia ndio iwe mwisho. Hizi elimu za 'copy and paste' ndio shida. Kosa likifanyika pasichukuliwe hatua haimaanishi likijirudia lisichukuliwe hatua.

    ReplyDelete
  14. Kwa hiyo mnachagua wapi pa kufuata kanuni na wapi pa kutofuata kanuni?Mantiki ya kijinga haswa.

    ReplyDelete
  15. Me siafiki kilichofanywa na TFF ila hakuna mtu hata mmoja mwenye kujua sababu ya hili so far hata hivyo nachojiuliza ni kwamba yanga wangepoteza nn kusubiri masaa matatu zaidi ili wamalize kazi waliyoiandaa kwa siku 8?
    Badala yake wanajisifu kuwa wamefuata kanuni na sheria huku mashabiki wao wengi wakilalama eti mechi zao tu ndo zinazofanyiwa mabadiliko utadhani timu inacheza yenyewe!
    Tuliokuwa na haki ya kulalama sana ni mashabiki tuliokuwa uwanjani kwakuwa kila mmoja alikuwa na ratiba na bajeti yake binafsi ila viongozi na timu walipaswa kutopaniki kabisa kama ilivyokuwa kwa upande wa simba!

    ReplyDelete
  16. Tuache kuzingumza kishabiki. Tuangalie hatuna ya mpira wetu. Hebu nijuze na ujiulize Sheria unasemaje kama timu moja haita yikes uwanjan nini kifanyike? Na yule ambaye hajatokea anapswa kufanyiwa nn? Kama kweli kwenye Hulu Saka Simba alikuwa na haki kwa nn wasingempa ushindi wake kwa nijibu wa Sheria. Na badala yake wameanua kughairi mechi. Tujiulize kwa nn imetokea ivi. Na Kuna nn nyuma ya hilo.

    ReplyDelete
  17. Wa Tanzania tuache mazoea,

    Kanuni za Fifa zinasema taarifa itolewe si chini ya masaa 24, TFF walitumia kanuni ipi?
    Au mnatetea TFF bila ya kuwa na uhakika na mnachosema?
    Ndio maana mpira wetu hauendelei, figisufigisu nyingi

    ReplyDelete
  18. Tff wanafanya upuuzi mnabaki kuwa chekea, lazima wakemewe vinginevyo watazidi kudidimiza soka letu.

    ReplyDelete
  19. Acheni zuga yenu, simba ndio TFF

    ReplyDelete
  20. Hawa wanaofanya wanavotaka na wakiachiliwa hivo hivo basi wengine Watauga na fujo itakuwa tabu kukontirol. Shida yao ni kukosa ubingwa kwa miaka mine na kuiona Simba jinsi inavostawi na kumetulia na kuchukuwa ubingwa kwa mara nne mfululizo na huku wakikata mbuga kombe la clubs Africa kuzidhinda timu kama vile Al Ahli na kila wakiona uchungu ndivo wanaozidi kuanguka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic