May 4, 2021


 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama leo Mei 4, amekabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Tuzo hiyo alishinda baada ya kuwashinda wachezaji wenzanke wawili ambao ni Aishi Manula na Shomari Kapombe ambao walitinga hatua ya fainali.

Amekabidhiwa leo katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Mo Simba Arena wakati wa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Mei 8.

Chama amesema kuwa kupata tuzo hiyo kunamuongezea morali na nguvu ya kufanya kazi kwa uzuri zaidi kwa ajili ya mechi zao zijazo.

"Ni furaha kwangu kupata tuzo ninaona kwamba inaongeza morali kwangu na wachezaji wengine kuzidi kupambana kufanya vizuri.

"Katika hili ninawapongeza wachezaji wenzagu kwa sapoti pamoja na mashabiki ambao wamekuwa pamoja nasi, kikubwa waendelee kutupa sapoti," amesema.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Chama ni kinara wa pasi za mwisho akiwa ametoa jumla ya pasi 13 na amefunga mabao 7 kati ya 58 yaliyofungwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic