IMEELEZWA kuwa, maisha ya nyota wazawa wawili Miraj Athuman ambaye ni kiungo mshambuliaji na Said Ndemla ambaye ni kiungo mkabaji ndani ya kikosi cha Simba, kwa sasa ni magumu kutokana na Kocha Mkuu, Didier Gomes kushindwa kuelewa juu ya uwezo wao.
Kwa sasa kikosi cha Simba kipo nchini Afrika Kusini ambapo kinajiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali unaotarajiwa kuchezwa Mei 15, mwaka huu.Katika nafasi ya kiungo mshambuliaji, Luis Miqussone raia wa Msumbiji amekuwa chaguo la kwanza, huku kwa ukabaji akiwa ni Mganda, Taddeo Lwanga jambo linalomaanisha uwepo wao umechukua namba za wazawa hao.
Katika msafara uliokwea pipa Mei 11 kwenda Afrika Kusini, nyota hao wawili hawakuwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 waliosajfiri.
Mtoa taarifa kutoka Simba, aliliambia Spoti Xtra kwamba: “Ndemla na Miraji wamebaki, kwa sasa nafasi zao ndani ya Simba ni ngumu sana hasa kutokana na sera ya mwalimu kuwakataa, hivyo lolote linaweza kutokea kwao.”Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kuwa sababu ya nyota hao kuachwa haiwezi kuwekwa wazi kwa sasa.
Tatizo wachezaji wazawa hawajitumi.Inabidi msimu ujao wakina Ajibu,Miraji,Ndemla,Gadiel,Dilunga watafute timu za kwenda maana Bila hivyo wakilewa sifa za kuandika magazetini watazidi kusugua bench
ReplyDeleteWanapaswa kukaza zaidi mazoezini ili waweze kumshawishi kocha kuwapatia nafasi
ReplyDeleteAaaaah wee Ndemla yuko poa na Miraji yuko fresh tu. but sijui tu
ReplyDelete