KOCHA wa makipa wa zamani wa Yanga, Manyika Peter amesema kwa namna ambavyo Simba wanavyocheza ni ngumu kukabiliana nao kwa sababu uwezo wao kwa sasa ni mkubwa zaidi ya wachezaji wengi ligi kuu.
Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana leo, Jumamosi Mei 8, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Manyika ambaye aliwahi kutamba na kikosi cha Taifa Stars miaka ya nyuma, alifunguka kuwa Simba ina wachezaji wengi bora ambao wakati wowote wanaweza kuipa matokeo timu yao na kuongeza kuwa akili yao kwenye soka imekuwa pana zaidi.
Akizungumza na Championi, Manyika alisema wapo wachezaji wa Simba wakiwa uwanjani wanakimbiambia bila kuwa na mpira ambapo watu kama hao huonekana kwenye matukio muhimu na ambayo hutengeneza hatari kubwa kwa timu pinzani.
“Simba kwa sasa wapo levo tofauti, wachezaji wao wengi ni bora tofauti na wengine wengi wanaocheza ligi kuu.
"Kuna watu wapo pale wanakimbia bila kuwa na mpira, ukiona wameshika mpira basi kuna madhara yanatokea timu pinzani,” alisema kocha huyo wa makipa wa Kagera Sugar.
Kagera Sugar ilipocheza na Simba mchezo wa Kombe la Shirikisho, ubao ulisoma Simba 2-1 Kagera Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment