May 30, 2021

 

UONGOZI wa kikosi cha klabu ya Yanga umekiri kuwa Mkata umeme wao Mkongomani, Mukoko Tonombe anazivutia klabu nyingi kubwa barani Afrika, ambazo zimeonekana kuhitaji huduma ya mchezaji huyo.

Mukoko ambaye amebakisha mwaka mmoja tu katika mkataba wake na klabu ya Yanga ameonekana kuzivutia baadhi ya klabu kubwa wakiwemo wababe wa soka kutokea nchini Guinea, Horoya ambao wanatajwa kuweka dau la zaidi ya Shilingi Milioni 400 za Kitanzania kwa ajili ya kupata huduma yake.

Mukoko akiwa katika msimu wake wa kwanza tu ndani ya kikosi cha klabu ya Yanga, amefanikiwa kuhusika katika mabao nane akifunga mabao manne na kuasisti mabao manne mpaka sasa.

Akizungumzia ishu ya dili la Mukoko, Mkurugenzi wa mashindano wa klabu ya Yanga, Thabit Kandoro amesema: “Ni kweli zimekuwepo baadhi ya timu kubwa barani Afrika, ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya kiungo mkabaji wetu Mukoko Tonombe.

"Hii inatokana na ukweli kuwa kiungo huyo amekuwa katika kiwango bora msimu huu."


7 COMMENTS:

  1. Milioni 400 nyingi wachukue watazitumia kusajiri wengine wazuri, mpira ni biashara

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wakifanikiwa kufanya biashara hii wanaweza pata majembe mawili ama matatu ya kazi

      Delete
  2. Mimiliomi Mia nne hamns kitu

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Hakuna kiungo bora tz kama mkoko tonombe wengine mbwa tu......Ukibisha weka takwimu hapo.....Manyau nyau

      Delete
    2. Upo sahihi ndiyo maana amewapa ubingwa, vyura nyie

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic