May 6, 2021


 HASARA kubwa inakwenda kutokea kwenye ulimwengu wa soka kwa sasa ikiwa hakutakuwa na uwekezaji utakaofanyika kwa ajili ya wakati ujao kutokana na mazingira ambayo tupo.

Ipo wazi kwamba kuna lala salama ambayo inaendelea kwa kila timu kupambana kufikia malengo yake huku zingine zikiwa kwenye mstari wa kushuka daraja.

Zile ambazo zinatoka Ligi Kuu Bara zitakapoibukia ndani ya Ligi Daraja la Kwanza zitakuwa na kazi ya kurudi tena msimu mwingine huku ambako zimetoka.

Ni timu nne ambazo zitashuka. Ikumbukwe kuwa huu ni msimu wa mwisho kwa timu kushuka nne kwa pamoja kutoka ligi kuu mpaka Ligi Daraja la Kwanza hivyo msimu ujao ni timu mbili ambazo zitashuka.

Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) lilikuwa na mpango wa kupunguza idadi ya timu kutoka 20 mpaka 16 ambapo ilianza msimu uliopita kwa kushusha timu nne na mbili zikacheza play offs.

Msimu huu pia zitashuka timu nne ili msimu ujao zibaki timu 16 ambazo zilikuwa zinahitajika. Hapa kuna hasara ambayo inakwenda kupatikana pia na faida haitakosekana.

Msimu uliopita nne na msimu huu nne hivyo ni jambo ambalo lipo na halitakwepeka muhimu kwa timu zote kupambana.

Faida yake ligi itakuwa inachezwa wikiendi mpaka wikiendi na tutaepuka ile ratiba ngumu ambayo ilikuwa inafanyika wakati huu kulipokuwa na timu 20.

Hali ikiwa hivi maana yake ni kwamba mwalimu atapata muda wa kutengeneza timu na kufanyia kazi makosa ambayo watakuwa wameyafanya kwenye mechi zao ambazo zimepita.

Itakuwa ni tofauti na kucheza leo na kesho unapumzika kisha siku ijayo anakuwa na kazi ya kuongoza timu kwenye mchezo mwingine kusaka ushindi.

Hata yale makosa ambayo yametokea kwenye mchezo wao uliopita inakuwa ngumu kwa mwalimu kufanya marekebisho ili aweze kupata matokeo wakati ujao huwa inakuwa ngumu.

Kwa kuwa kutakuwa na mechi kwa muda basi itakuwa ni rahisi kwake kupanga mpango kazi makini utakaompa matokeo chanya.

Atapata muda wa kutazama makosa yaliyopita na kuyafanyia kazi. Jambo hilo litamfanya awe kwenye malengo yake muda wote bila mashaka.

Pia wachezaji watapa muda wa kupumzika kwa sababu watakuwa wana muda wa kujipanga na kujiandaa kwa mechi ijayo bila ratiba kuwabana.

Mechi ijayo watacheza kwa nguvu kubwa kwa kuwa watakuwa na ari mpya baada ya kupata muda wa kupumzika. Hiyo itafanya waweze kuonyesha ushindani na uwezo wao ambao wanao.

Tofauti na awali ilikuwa mechi ikikamilika moja hapo hakuna muda mrefu wa mapumziko zaidi ya kuunganisha kwa ajili ya mechi ijayo.

Jambo hilo lilikuwa linawafanya wachezaji kucheza chini ya kiwango na muda mwingine kucheza wakiwa katika hali ya uchovu katika kusaka ushindi.

Hilo halikuwa jambo jema kwa benchi la ufundi, mashabiki na wachezaji kwani wote furaha yao ni kuona wanapata matokeo ila mwisho wa siku haikuwa hivyo.

Ukiachana na hayo, hasara inakuja kwenye upande wa kupunguza wigo mkubwa wa wachezaji ambao walikuwa wanashiriki Ligi Kuu Bara pale ambapo wanaondoka katika utawala kwa wakati mmoja.

Ukweli ni kwamba wigo wa wachezaji wengi wataondoka na wataibukia Ligi Daraja la Kwanza. Wapo wengine ambao watakuwa nje ya soka kwa kuwa wataamua kufanya mambo mengine.

Unapozungumzia timu nne ambazo zinashuka, hapo kuna wachezaji zaidi ya 40 ambao wanaondoka kwenye mfumo wa ligi mpaka Ligi Daraja la Kwanza kuanza maisha mapya.

Hapo kutakuwa na wachezaji wengi ambao wataondoka hapo. Hilo ni lazima litazamwe kwa ukaribu na mamlaka husika yaani TFF ili kujua namna gani itawezekana kulinda vipaji hivyo.

Kuna wachezaji ambao hawataonekana kwa msimu ujao kwenye ligi kwa kuwa timu zao zitakuwa zimeshuka na wana uwezo ambao ulikuwa ni faida kwao na taifa kiujumla.

Wengine watakwenda Ligi Daraja la Pili wale ambao wanatoka Ligi Daraja la Kwanza hivyo kuna hasara ambayo inabidi TFF ijiandae kuipokea.

Jambo la kufanya TFF iwekeze huku pia kwenye Ligi Daraja la Kwanza na isipepese macho katika utendaji ni lazima kuwe na mfumo bora ambao utasaidia hawa ambao watashuka kubaki katika soko.

Hizi ni busara za Seleman Matola


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic