OFISA Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa hakuna anayeweza kumpangia majukumu Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes katika utendaji wake wa kazi.
Hayo ameyasema ikiwa ni baada ya kuenea kwa taarifa kwamba wakala wa mchezaji wa Meddie Kagere, Patrick Gakumba kudai kuwa mteja wake hapewi nafasi kikosi cha kwanza kucheza.
Msimu huu wa 2020/21 maisha ya Kagere kikosi cha kwanza yamekuwa ni ya kuunganisha licha ya kwamba ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao 11.
Gomes amekuwa akipenda kumtumia Chris Mugalu na wakati mwingine kutumia viungo katika kufanya mashambulizi.
Manara amesema:"Nimeona kwamba kwenye mitandao ya kijamii inaeneza taarifa kuhusu wakala wa Kagere akidai kwamba mchezaji wake hachezi hilo sio sawa na hakuna ambaye anayeweza kumpangia majukumu kocha.
"Ikiwa ni wakala wa mchezaji basi anapaswa apambane kuhusu stahiki za mteja wake labda ingekuwa sawa ila kuhusu kupewa nafasi ya kuanza ma kutoanza hilo ni jukumu la kocha,".
Ila asipocheza kwenye hizi mechi zilizobaki atapoteza kiatu chake cha ufungaji bora.wakati mwingine tunapaswa kukubali pale tunapokosolewa.
ReplyDeleteManara amekimbilia kujibu hapa inapaswa ama itoke kauli ya CEO au bodi ya ligi
DeleteBODI YA LIGI TENA? IANHUSIKA NA NINI KUHUSU KAGERE KUTOCHEZA?
DeleteKweli usemayo maana huwezi kumpangia kocha mchezaji, yeye anajua Fitness ya mchezaji na aina ya mechi, mbona south aliingia sub
ReplyDelete