NAHODHA msaidizi wa kikosi cha Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa licha ya timu hiyo kuwa na matokeo yasiyotabirika katika michezo ya hivi karibuni, bado hawajakata tamaa katika malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu huu
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya pili na Simba inaongoza ligi wote wamejikusanyia pointi 61 tofauti ikiwe ni mechi za kucheza kwa Simba na Yanga.
Yanga imecheza jumla ya mechi 29 na Simba imecheza jumla ya mechi 25 kwa msimu wa 2020/21.
Yanga wamekuwa na mwenendo wa kusuasua ambapo katika michezo nane mfululizo iliyopita wamefanikiwa kushinda michezo mitatu pekee, wamepoteza miwili na kutoa sare kwenye mechi tatu.
Matokeo hayo yameonekana kuzidi kuwapunguza kasi Yanga katika vita ya kuwania ubingwa wa msimu huu.
Akizungumzia mipango yao Mwamnyeto amesema: “Ni kweli tumekuwa na mwendo wa kusuasua kwenye michezo yetu iliyopita, lakini tunaamini kuwa hiyo ni hali ya kawaida na ni suala ambalo tayari linafanyiwa kazi na benchi letu la ufundi.
“Hivyo, tunapambana kuhakikisha tunafikia malengo yetu msimu huu ikiwemo kumaliza katika nafasi za juu, na hata kutwaa ubingwa.”
0 COMMENTS:
Post a Comment