May 22, 2021


 MPANGO namba moja wa Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes leo mbele ya Kaizer Chiefs ni kupindua meza kibabe ili kuweza kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Kaizer Chiefs katika mchezo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ubao wa FNB ulisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba na lilipopachikwa bao la nne, Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs, Gavin Hunt alionekana akicheka.

Hiyo ilikuwa ni Mei 15 katika mchezo wa raundi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Habari zimeeleza kuwa jambo hilo limempa hasira Gomes hali iliyomfanya aanze maandalizi mapema akiwa nchini Afrika Kusini na aliporejea na kikosi Bongo kazi ilikuwa inaendelea.

“Kile kicheko cha yule kocha kimewaumiza wengi mpaka Gomes mwenyewe hajapenda, sasa kazi ilianzia nchini Afrika Kusini wachezaji walianza mazoezi na hata waliporudi Tanzania waliendelea na mazoezi bila kupumzika, sasa kilichobaki ni dakika 90 uwanjani,” ilieleza taarifa hiyo.


Gomes aliliambia Championi Jumamosi kuwa wamekasirika kufungwa ugenini hivyo watapambana kupata matokeo wakiwa nyumbani kwenye mchezo wa marudio.


“Kupoteza mchezo wa kwanza ugenini kwetu ni hasara ila kwa kuwa imetokea sasa tunajipanga kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio, tutakuwa nyumbani hakuna kitakachoshindikana tutafanyia kazi makosa ili kupata ushindi,” alisema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic