June 21, 2021


KIUNGO wa Simba, Luis Miquissone rekodi zinaonyesha kuwa mguu wake wa kushoto umefunga mabao mengi ambayo ni 6 huku ule wa kulia ukiwa umetupia bao moja sawa na lile alilofunga kwa kichwa.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ikiwa imetupia jumla ya mabao 65 kiungo huyo ametupia jumla ya mabao 8 pia ametengeneza pasi za mwisho 10.

Katika mabao hayo 8 Luis amefunga Uwanja wa Mkapa mabao matano ambapo alitupia mbele ya Azam FC dk ya 78 kwa mguu wa kushoto akiwa nje ya 18 pia mbele ya  JKT Tanzania alipachika bao dk 37 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18. Mbele ya Dodoma Jiji dk ya 55 ndani ya 18 guu la kushoto.

Guu lake la kulia alifunga bao moja ilikuwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni mbele ya Mtibwa Sugar dk 68, akiwa ndani ya 18.

Pia kwa kutumia kichwa nyota huyo alitupia bao moja ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons alipachika bao dk 90 akiwa ndani ya 18.

Nje ya Dar ametupia mabao matatu ilikuwa mwendo wa mojamoja  mbele ya JKT Tanzania dk 53 nje ya 18 kwa mguu wa kushoto, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma,  mbele ya Kagera Sugar, dk 12 kwa mguu wa kushoto ndani ya 18, Uwanja wa Kaitaba , mbele ya Polisi Tanzania, dk 28 mguu wa kushoto ilikuwa nje ya 18 Uwanja wa Kirumba.

 

 

3 COMMENTS:

  1. Hutu jamaa anajitahidi sana, hatushangai huwa anakamiwa mno na mabeki, ila ni mstaarabu sana.

    ReplyDelete
  2. Na hayo yote yanatokana na nidham, juhudi, akili na utiifu wa hali ya juu ndio sababu ya natunda hayo na iwe somo kubwa kwa wite

    ReplyDelete
  3. Wachezaj wa kibongo wangekuwa na nidhamu ya miquissone wangefanikiwa sn binafc na taifa. Shda bhn wachezaji wetu wa kibongo wakishajua kuwa wanajua....,, doh! Shda tupuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic