June 21, 2021


 TIMU ya Barcelona imezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha dili la miaka miwili kwa mshambuliaji Memphis Depay kutoka Lyon.

Timu hiyo ilikuwa inaipigia hesabu saini ya nyota huyo kwa muda mrefu na mwisho wa siku walifanikiwa kumpata mchezaji huyo na kumpa dili la miaka miwili ataondoka hapo mwaka 2023 ikiwa mabosi hao hawatakuwa tayari kumpa dili jipya.



Staa huyo alijenga jina lake akiwa ndani ya Manchester United kabla hajatua Lyon hivi karibuni aligoma kusaini dili jipya na timu hiyo ya Ufaransa.

Anakuwa ni mchezaji wa nne Barcelona inayonolewa na Kocha Mkuu, Ronald Koeman kusajiliwa kwenye usajili huu baada ya kuanza na Sergio Arguero, Eric Garcia na Emerson Royal.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic