June 1, 2021


KLABU ya Simba, inafikiria kusitisha mkataba wa kiungo wake mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Perfect Chikwende huku ikipanga kumuongezea mkataba Francis Kahata.

 

Mkataba wa Kahata unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili.

 

Simba ilimsajili Chikwende katika usajili wa dirisha dogo msimu huu maalum kwa ajili ya Ligi Kuu Bara, akichukua nafasi ya Kahata ambaye yeye aliwekwa maalum katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Simba inafikiria kuachana na Chikwende baada ya kushindwa kuonyesha ushindani katika kikosi cha Mfaransa, Didier Gomes.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mshambuliaji huyo amepoteza nafasi ya kucheza katika kikosi, pia kukaa benchi la wachezaji wa akiba.

 

Aliongeza kuwa, uongozi huo hivi sasa unafikiria kumuongezea mkataba Kahata ikiwezekana arejeshwe katika kikosi cha wachezaji watakaocheza ligi kuu na mashindano mengine msimu ujao akichukua nafasi ya Chikwende.

 

“Kilichotokea kwa Chikwende kila kiongozi hakitegemei ni baada ya kushindwa kuonesha kile ambacho walichokuwa wanakihitaji baada ya kutua Simba.


“Hivyo uongozi unafikiria jinsi ya kuachana naye, lakini wanapata ugumu wa kusitisha mkataba wake kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho watatakiwa kumlipa kutokana na muda wa mkataba ambao ameusaini.

 

"Upo uwezekano mkubwa wa Simba kumuongezea mkataba Kahata, kwani yeye tayari alikuwa amezoea mazingira ya ligi hapa nyumbani tofauti na Chikwende ambaye amefeli,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Mkuu wa Mahudhui wa Simba, Ally Shatry kuzungumzia hilo, alisema: “Masuala yote ya usajili hivi sasa yapo chini ya Bodi ya Wakurugenzi wa Simba na siyo kwangu," .

 

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, hivi karibuni alizungumzia usajili na kusema: “Suala la usajili hivi sasa tumeliachia benchi la ufundi ndiyo ambalo linajua mchezaji gani wa kusajiliwa na kuachwa, sisi viongozi kazi yetu utekelezaji tu.

6 COMMENTS:

  1. Mpira wa Kibongo hautakuja kuendelea,Chikwende ni mchezaji mzuri Sana sema coach hampi nafasi.Angepewa match za kutosha tungesema ameshindwa kuonyesha makali.Hapo wajanja washapiga pesa kwa utapeli.Mungu tunusuru na kirus hiki Cha matapeli wa mpira


    ReplyDelete
  2. Mpira wa bongo ni kichefuchefu.Mtu hapangwi wanasema ameshindwa kuonyesha kiwango.Ngoja nishabikie Chelsea fc, maana ujanja ujanja tushauchoka wa wapiga dili

    ReplyDelete
  3. Chikwende hakua kwenye mpango, ilikua zoazoa tu asije chukuliwa na Yanga, ndio maana hata hatumiki

    ReplyDelete
  4. Mpira wa Tanzania unaweza kuufananisha na mtu anae taka utajiri kupitia njia za waganga. Haswa zile njia za harakaharaka, ndo maana hata makocha hawakai muda mrefu.simba ilitakiwa wampe tu muda chikwende Kama wanavyopewa akina chama na Luis ili nayeye apate physicality ya mpira.

    ReplyDelete
  5. Chikwende ameshindwa kuperfom hata akiondoka kahata arudi

    ReplyDelete
  6. Kwan amecheza mechi ngapi mpka waseme hajaonesha kiwango ndo matatzo ya kumchukua mchezaji kwa kuangalia performance ya mechi moja na hilo ndo linaharibu Moira wetu Chikwende n mchezaji mzuri sana sema hapewi nafasi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic