ZOEZI la kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi za uongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) limezidi kuendelea ambapo leo pia Juni 11 wagombea wamejitokeza kuchukua fomu.
Miongoni mwa waliochukua fomu ya kugombea Urais ni pamoja na Hawa Mniga ambaye anakuwa ni Mwanamke wa kwanza kuchukua fomu hiyo.
Hawa ni mdau wa soka Tanzania na amewahi kuwa katika kamati ya ajira ndani ya TFF.
Mpaka sasa ambao wamechukua fomu kuwania nafasi ya Urais TFF imefika tisa ikiwa ni pamoja na Deogratius Mutungi, Ally Mayay, Evans Mgeusa, Oscar Oscar, Tarimba Abbas, Hawa, Wallace Karia, Ally Saleh na Zahir Mohammed Haji.
Leo Juni 12 ni mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea.
0 COMMENTS:
Post a Comment