KWA kiasi fulani, taarifa za aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, kukosekana katika Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Jumapili hii, zinaweza kuwa mbaya kwa wapenzi na wanachama wa klabu hiyo.
Hatua hiyo inakuja baada ya Manji kurejea nchini hivi karibuni na kuleta matumaini kwa Wanayanga waliotarajia kumuona katika mkutano huo uliopangwa kufanyika Ukumbi DYCCC, Chang’ombe, Dar.
Yanga katika mkutano huo miongoni mwa ajenda zake zitakuwa ni mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kwenda katika mfumo wa kisasa.Hivi karibuni, ziliibuka taarifa za Manji kulipia kadi ya uanachama ya klabu hiyo ambayo ingemruhusu kushiriki mkutano mkuu, lakini watu wake wa karibu, wamekanusha uwepo wa taarifa hizo.
Mtu wa karibu na Manji, amelithibitishia Spoti Xtra kwamba, kigogo huyo ataondoka nchini kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, huku akiweka wazi kwamba, kiongozi huyo hakulipia kadi yake ya uanachama tangu atue nchini.
“Manji hakulipia ile kadi ya uanachama kama ambavyo watu wanasema, mwenyewe kabla ya mkutano mkuu kufanyika, atakuwa ameshaondoka hapa nchini, hivyo ni ngumu sana kwake kuwepo siku hiyo,” alisema mtu huyo.
Taarifa za Manji kukosekana katika mkutano huo, zitawashtua Wanayanga ambao wamekuwa na mapenzi makubwa na kiongozi wao huyo wa zamani ambaye hivi karibuni alirejea nchini baada ya kuondoka kwa muda mrefu kwani walipanga kumjadili kurudi kwake.
Manji aliwahi kuwa kiongozi wa Yanga kwa takribani miaka saba kuanzia 2012 hadi 2017 ambapo aliifanya timu hiyo kuwa tishio akifanikisha kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo kuanzia 2014 hadi 2016.
Wapenzi wa yanga wanaenjoy mno kupigwa changa la macho. Kama ktk usajili hata hili suala manji watu waliamua kuwachota wanayanga kwa kumlipia manji kadi yake na kuisambaza mtandaoni. Yakowapi sasa
ReplyDeleteUkweli marhabiki wa uto ni ziro ndiomana ata leo hii wakiambiwa chama amalizana na uto utawakuta mtaani wanashangilia duu, wamekuwa limbukeni
ReplyDeleteKumbe unataka wajibu wa mikia tu unadanganya na unaichafua sana yanga unatumika na hautaweza
DeleteBado na kesi ya Morison mpaka ligi inaisha bado haijasikilizwa
DeleteHii timu yetu msingi wake ni kudanganyana na hali hii inatupelekea kutokuwa na imani nayo. Manji hayupo nchini na hakulipia ada ya uwanachama na hio kurejea yanga halipo na sisi mambwege tukasadiki na
ReplyDeletekusherehekea. Naamini hili limefanywa makusudi kwa nia ya kuivuruga timu. Sherehe ilikuwa kubwa sana na kuwafanya wale wanaoitumikua timu na kuigharamia kwa mabilioni kwa upendo ndani ya roho zao kujiona hawathaminiwi na anayesherehekewa na kuwekwa upande hata kabla ya kufika kusiko na ukweli. Kikulacho kipo nguoni kwako.
Ndio ushamba wa watu wa mikia mabadiliko anayasimamia nani muwenaakili mabadiliko yatafanyika awepo na asiwepo simba fanyeni ya kwenu hamuta iangusha yanga na waandishi wenu takataka manara kasema
ReplyDeleteTunaelekea kwenye mechi za kufa na kupona kutokana na haya nini itakuwa morali ya za mashabiki na wachezaj. Jambo hili litazamwe kwa macho mawili tuwaone wachawi ambao mchana watu na usiku wachawi
ReplyDeleteManjii atarudi msijal wana uto, na akirudi na anarudi na zile baki tu baki.... Hahahaa
ReplyDeleteTatizo la mikia wao muda wote wanawaza Yanga, sasa hata wao Akiondoka Yule muhindi wa 20B za mali kauli hawana wanachakufanya,
ReplyDeleteLkn haishangazi kwasababu akili za masikini sikuzote kutengeneza majungu tu, ili watu wote walingae
Masikini siku zote wanaroho za husda
ReplyDelete