HUENDA beki wa Klabu ya Real Madrid, Sergio Ramos akaibukia ndani ya Klabu ya PSG msimu ujao wa 2021/22.
Tayari mabosi wa Real Madrid wametangaza kuachana naye baada ya dili lake kumeguka msimu huu hivyo dili likikamilika atajiunga na mabosi hao bure.
PSG inaelezwa kuwa imepeleka ofa kwa wakala wa mchezaji huyo mwenye miaka 35 na amekaa Madrid kwa muda wa miaka 16.
Taarifa zimeeleza kuwa muda wowote kuanzia sasa, Ramos atakwenda nchini Ufaransa kwa ajili ya kusaini dili jipya.
0 COMMENTS:
Post a Comment