June 1, 2021


IPO wazi kwamba kasi ambayo walianza nayo Mwadui FC ilikuwa inaonyesha kwamba kuna jambo ambalo litawatokea kabla ya msimu kuisha hatimaye limekamilika.


Haikuwa na mwanzo mzuri kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ukata na wachezaji walikuwa wanapitia mazingira magumu kwa kushindwa kulipwa stahiki zao kwa muda wa miezi kadhaa ila wakawa wanapambana.



Mwisho wa siku kwa sasa inakamilisha ratiba ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa itashiriki msimu ujao Ligi Daraja la Kwanza na ina mechi ambazo itacheza kwa sasa kukamilisha msimu wa 2020/21.


Weka kando Mwadui FC, tukumbushane kidogo kuhusu Simba ambao walikuwa ni wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kwa kasi ambayo walianza nayo kila mmoja aliamini kwamba wanakwenda kutimiza lengo lao la kutinga hatua ya nusu fainali.


Kosa la kwanza ikawa ni kiburi kosa la pili ikawa ni kiburi na kosa la tatu ikawa ni kiburi hapo ndipo anguko lao lilipotokea na ndoto yao kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa ikayeyuka.


Nasema hivyo kwa sababu niliongea awali kabisa kuhusu kuona anguko la Simba ikiwa watajiamini kupita kiasi. Niliwakumbusha habari za UD Songo na kuongea mambo mengi ya kufanya hasa kikubwa niliweka wazi kwamba nidhamu inahitajika.


Haikuwa rahisi kueleweka na mashabiki wengi wa Simba walicheki na mimi na kusema kwamba ninazingua na mengine kadhalika ila mwisho wa siku kila kitu kikawa wazi.


Kwa hatua ambayo wamefika msimu huu bado Simba wanastahili pongezi lakini wangekuwa na nidhamu na kuacha kiburi wakiwa wanapambana na wapinzani wao basi leo gii tungekuwa tunazungumza habari nyingne.


Ukiachana na Simba kwa sasa timu tatu zinapambana kushuka daraja na msimu ujao ziweze kushiriki Ligi Daraja la Kwanza, hili haliepukiki.


Miongoni mwa timu hizo ni pamoja na JKT Tanzania, Coastal Union,Gwambina hizi zipo kwenye ule mstari mwekundu lakini pia Mbeya City, Kagera Sugar, Ihefu, Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting, Dodoma Jiji mpaka Namungo.


Zote hizi hazipo sehemu salama hivyo ikiwa watashindwa kuwa na nidhamu katika yale ambayo wanayafanya anguko kubwa kwao linakuja.


Coastal Union ilikuwa kwenye mwendo mzuri ila ghafla mambo yamekuwa magumu ikiwa wataendelea kuwa na kiburi basi anguko kwao linakuja.


JKT Tanzania, bado mwendo wao ni kusuasua ni muhimu kuongeza nidhamu na kupambana kwa hali na mali kutimiza malengo yao.


Timu zote nina amini kwamba zikiweka nidhamu katika kupambana na kuachana na kiburi cha mafanikio basi watapata kile ambacho wanastahili.


 


 


 


  

9 COMMENTS:

  1. Spaonini kabisa pale walipoanguka Simba na Wala hakionikani hicho kiburi, isipokuwa walipigana na walifanya vizuri Sana na kupata sifa kutoka kwingi Duniani na kuziwezesha timu nyengine Tatu kushitiki msimu ujao. Mpira ndio ulivo. Simba ilijitshidi Sana lakini kufuzu na kutokufuzu kumo katika mikono ya Mungu Mtukufu na tunamshukuru hapa tulipofikia. Timu imetulia shuwsri kabisa bila ya chokochoko zozote Wala masikitiko au kushitakiana kusokwisha

    ReplyDelete
  2. Simba haijaanguka. Kucheza ligi ya klabu za Afrika halafu mkawa miongoni mwa klabu nane zilizobaki, ni hatua kubwa sana na sidhani kama ni sahihi kusema wameanguka

    ReplyDelete
  3. Yaani una ujasiri wa kusema kwamba Simba waliishia robo fainali kwa kuwa hawakukusikiliza wewe!?

    ReplyDelete
  4. Sidhani kama Huyu mwandishi hata kama anajua alimaanisha nini au ameandika nn? Kwahiyo hizo timu zisingekua na kiburi zingekua juu ya Kina namungo na biashara? Halafu huko chini ndio wangekua namungo biashara na ruvu shooting? Kila mwaka lazima kuwa na timu zinazofanya vizuri na nyengine vibaya na mwaka huu imekua bahati mbaya kwa hizo timu. Kuhusu simba sidhani kama hata unaijua simba maana hawajawahi kuidharau kaizer chiefs labda kama mwandishi ulikua Una list yako au ulitaka ucheze wewe. Simba walicheza na timu kubwa na matokeo ndio yale sasa sijui utuambie dharau gani uliiona

    ReplyDelete
  5. Mwandishi nia yako ni njema japo ukituma neno kiburi unamaanisha mengine. Kujiamini si kiburi. Kuna vitu huwezi kuvilinganisha. Huwezi linganisha Man U na Azam. Huwezi linganisha Mgahawa na Hotel. Simba walifanya makosa ya kimpira kwa kutojua nguvu ya mpizani wake na watumie mbinu ipi. Simba mafanikio waliyofikia ni makubwa sana na ya kupongezwa. Kufikia 8 bora Afrika si jambo la kufananisha na Coastal.
    Ungelinganish Coastal na timu za ligi kuu ningekuelewa. Kwa maana ya michezo ya Simba ligi kuu. Ungesema pia timu nyingine zilizoanza vizuri kwa kuongoza ligi kama Yanga na sasa hawaongozi na ukatoa mifano ya timu klabu bingwa zilizoanza vema na hazikumaliza vema ningeelewa. Japo najua umeandika kwa uchungu kama mshabiki wa Simba ambae ulitamani wapate ubingwa.

    Nikisoma vizuri naona umeandika ya Simba zaidi ya Coastal japo lengo lako lilikuwa kuandika ya Coastal. Mahali ambapo nakuelewa ni kwamba nia yako ilikuwa kusisitiza kuhakikisha timu hazipotezi dira na kuyaishi maono.

    ReplyDelete
  6. Kama kujiamini kiburi basi akili nazo zina viburi

    ReplyDelete
  7. Mamelodi alitolewa na Al Ahly nacho ni kiburi?.Football ni mipango hasa kumjua vizuri mpinzani wako.Unapofanya makosa kwenye football lazima uadhibiwe.Waandishi mjitahidi kua competent kwenye hoja ili kutokuonesha ushabiki wa wazi.

    ReplyDelete
  8. huyu jamaa ni chizi fulan analopoka ovyo ovyo ivo hajui maana ya mpira

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic