June 21, 2021


 MATESO Wadiba Kocha Msaidizi wa Mbeya City amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao Simba ila kesho watapambana kupata pointi tatu muhimu.

Mbeya City iliyo nafasi ya 13 na pointi 36 ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes iliyo nafasi ya kwanza na pointi 70.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wadiba amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao hivyo wataongeza nidhamu kwenye mchezo wao.

"Tunawaheshimu Simba kwa kuwa ni timu kubwa na inafanya vizuri haina maana kwamba tutawahofia hapana tupo tayari na tunaamini kwamba tutapata pointi tatu.

"Mchezo wetu uliopita tulipoteza hivyo mbinu mpya tutakuja nazo ili kuweza kupata matokeo chanya na imani yetu ni kuona tunashinda mashabiki watupe sapoti," amesema.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Sokoine Mbeya City ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kuziacha pointi tatu mazima.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic