BAADA ya kufanikiwa kusimama langoni kwenye michezo 13 bila kuruhusu bao yaani ‘Clean Sheet’, mlinda mlango wa kikosi cha Mtibwa Sugar, Aboutwalib Mshery amefunguka kuwa malengo yake makubwa msimu huu ni kuhakikisha anamaliza utawala wa misimu mitano wa kipa wa Simba, Aishi Manula kwa kutwaa tuzo ya kipa bora wa msimu.
Kwa misimu mitano mfululizo iliyopita kuanzia msimu wa 2015/16 mpaka 2019/20, Manula amekuwa mmiliki wa tuzo ya golikipa bora wa msimu ambayo hutolewa kwa kipa aliyefanya vizuri zaidi.
Mpaka sasa Mshery akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar msimu huu, amefanikiwa kusimama langoni katika michezo 13 bila kuruhusu bao lolote, huku Mtibwa ikiwa imesaliwa na michezo miwili kukamilisha michezo yao ya Ligi kuu kwa msimu huu.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mshery alisema: “Namshukuru Mungu kwa kuwa na wakati mzuri msimu huu, ambapo mpaka sasa nimefanikiwa kuwa na ‘clean sheet’ 13, lakini malengo yangu makubwa ni kuhakikisha napambana zaidi kuhakikisha namaliza msimu nikiwa na clean sheet nyingi zaidi ambazo zitaniweka katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya golikipa bora wa msimu huu," .
0 COMMENTS:
Post a Comment