June 21, 2021

 


JINA la mshambuliaji wa Yanga, Fiston Abdulazack imeelezwa kuwa limekatwa jumlajumla hivyo hatakuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.

Mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa Burundi chaguo la aliyekuwa kocha wa timu hiyo msimu huu Cedric Kaze amekuwa na mwendo wa kusuasua jambo ambalo limewafanya mabosi wa Yanga kukubaliana kuachana naye.


Alipoibuka ndani ya Yanga alipewa dili la miezi sita lenye kipengele cha kuongeza mkataba ikiwa kiwango chake kitaimarika ila imekuwa tofauti na vile ambavyo walifikiria.

Ndani ya ligi ametupia bao moja na pasi moja pia ana bao moja alilofunga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Ken Gold ilikuwa Uwanja wa Uhuru kwa mkwaju wa penalti.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika zimeeleza kuwa nyota huyo hayupo kwenye mipango ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi hivyo ataondoka.

"Fiston muda wake wa kuondoka umewadia baada ya kushindwa kwenda sawa na kasi ya Yanga, kwa namna yoyote ile ataondoka na hataongeza dili jipya," ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni, Fiston alisema kuwa hana furaha ya kuwa ndani ya kikosi hicho kilicho nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na pointi zake ni 67 na imefunga mabao 49.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic