TUZO ya Mchezaji Bora wa Mwezi Mei,aliyoipata mshambuliaji wa Azam, Prince Dube imewafunika mastaa wote wa Ligi Kuu Bara baada ya kuandika rekodi ya kuwa mchezaji pekee mpaka sasa msimu huu, ambaye amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo mara mbili.
Dube alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei baada ya kuwashinda Erick Mwijage wa Kagera Sugar na mlinda mlango wa Yanga, Metacha Mnata alioingia nao fainali, hii ni mara ya pili kwa Dube kutwaa tuzo hiyo, ambapo tuzo yake ya kwanza aliitwaa mwezi Septemba, mwaka jana.
Dube akiwa kwenye msimu wake wa kwanza tu ndani ya Azam kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara pekee, mpaka sasa amefanikiwa kuhusika kwenye mabao 19 ya klabu hiyo, akifunga mabao 14 na kuasisti mara tano.
Dube amesema: “Nimefarijika sana kwa kufanikiwa kwa mara nyingine tena kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.
“Kwangu hii ina maana kubwa sana, na napenda kuwashukuru wachezaji wenzangu wa Azam, benchi la ufundi na watumishi wote bila kuisahau familia yangu kwa kuendelea kuniamini.” amesema.
NCHI YA FUIGISU NA MAJUNGU, KATIKA MWEZI MWEI MCHEZAJI GANI AMENG'ARA ZAIDI KAMA SIO JOHN BOCCO. TOKA APRIL MPAKA MAY INAINGIA JUNE BOCCO AMECHEZA MMECHI 4 NA KUFUNGA MABAO 7. NANI AMEFANYA HIVYO MWINGINE?
ReplyDelete