PASCAL Mshindo, beki chipukizi wa Klabu ya Azam FC leo Juni 12 amesaini dili la miaka mitatu kuwa mchezaji wa kulipwa ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC kupitia ukurasa wao wa Instagrm imeeleza kuwa Pascal Mshindo ambaye alikuwa anacheza kwenye timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, amesaini mkataba wa kwanza rasmi wa miaka mitatu wa kuitumikia Azam FC kama mchezaji wa kulipwa.
Mshindo aliyepandishwa timu kubwa kutokea timu ya vijana (Azam FC U-20), ameshacheza mechi tatu za mashindano za Azam FC, akifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri.
Kwa kusaini mkataba huo, Mshindo ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2024.
Kwa kukamilisha dili la beki huyu wa kushoto anakuwa ni wa pili kumalizana na Azam FC na anauhakika wa kubaki hapo msimu ujao baada ya awali kutangaza kukamilisha dili la Edward Manyama ambaye naye amesaini dili la miaka mitatu.
Manyama alikuwa anakipiga ndani ya Ruvu Shooting ambapo awali ilielezwa kuwa amemalizana na Simba kisha mabosi wa Azam FC wakapindua meza kibabe.
0 COMMENTS:
Post a Comment