June 12, 2021

OSCAR Oscar ambaye ni mchambuzi wa masuala ya michezo Bongo pia akiwa ni mtangazaji wa E FM amesema kuwa anaamini kwamba ametimiza matakwa ya kanuni za fomu ya uchaguzi ambayo amewania ikiwa ni pamoja na elimu aliyonayo.

 Oscar anayewania nafasi ya Urais ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) amesema kuwa hajapata endorsment hata moja kwa kuwa kanuni inahitaji mgobea kupata kura tano kutoka kwa wanachama ambao wako zaidi ya 40.

Pia ameweka wazi kwamba shukrani kubwa kwa Waandishi wa Habari ambao walikuwa naye bega kwa bega katika kutoa taarifa. Ameongeza pia amekutana na changamoto kubwa ya kupata endorsment (wadhamini) ambayo ilikuwa ni tatizo kubwa kwake na hakupata endosment hata moja. 

 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic