Jumapili iliyopita ndani ya ukumbi wa DYCC Chang’ombe Dar es
Salaam, tukio jingine la historia nzuri liliandikwa kwa sauti moja kubwa ya
Wanachama wa klabu ya Yanga baada ya kuupitisha mchakato wa mabadiliko wa klabu
hiyo.
Hatua hii ni kubwa sana katika historia ya klabu ya Yanga
tangu kuanzishwa kwake mwaka 1935, na bila shaka hatua hii inawasogeza zaidi
katika ile Yanga ya ahadi iliyoanza kufikiriwa katika kikao cha mkutano mkuu wa
wanachama wa klabu hiyo uliofanyika Agosti 6, mwaka 2016.
Katika kikao hicho ambacho kilifanyika miaka mitano na miezi
10, iliyopita ndipo kwa mara ya kwanza lilikuja wazo la kukodishwa kwa klabu ya
Yanga kwa kipindi cha miaka 10 kwa kampuni ya Yanga Yetu iliyokuwa chini ya
aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.
Najua haikuwa safari rahisi kwa Yanga mpaka kufikia hatua
hii, kwani wamefanikiwa kuruka vikwazo vingi ili kuwa hapa walipo sasa, kuna
watu ambao waliwakatisha tamaa, kuwacheka na hata kusimama njiani ili kuwazuia,
lakini bado walipambana mpaka tone la mwisho la jasho kufika hapa.
Pongezi za pekee ziwaendee Mwenyekiti wa Yanga, Daktari
Mshindo Msolla kwa kupitisha maadhimio ya mchakato huu, lakini pia Uongozi wa
kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu ya Yanga kwa kutoa kiasi kikubwa cha
fedha kudhamini mchakato wote.
GSM walileta wataalamu kutoka kampuni ya La Liga ya nchini
Hispania, ambayo imehusika kwa kiasi kikubwa katika uandaaji wa rasimu ya
mabadiliko ya mfumo na ile ya kikatiba katika kufanikisha mchakato huu.
Kilichobaki kwa sasa ni kuhakikisha Uongozi unakuwa na
mpango mkakati thabiti wa kuhakikisha rasimu iliyopendekezwa inawekwa katika
utekelezaji wa kila siku ‘Operational Planning’ ili kufanikisha, na
kuukamilisha mchakato huu kwa muda uliopangwa.
Yanga inakuwa klabu ya pili hapa nchini kuuendea mchakato wa
uendeshaji wa klabu kisasa, ambapo tayari wapinzani wao wa jadi Simba tayari
wamelifikisha suala hilo kwenye meza ya Tume ya ushindani wa Biashara (FCC).
Mpira wa sasa ni biashara kubwa duniani, na ili kuendana na
ushindani wa soko la dunia ni wazi klabu zetu zinapaswa kufanya mabadiliko ua
kimfumo, na kutoa mianya kwa wawekezaji wengi zaidi kujitokeza kuwekeza ndani
ya klabu hizi.
Uwekezaji huu utazidi kuzipa klabu zetu misuli ya kuweza
kufanya usajili wa wachezaji bora zaidi, kuwatunza wachezaji hao katika
mazingira bora, na hata kutoa stahiki nono kama ambavyo klabu nyingine zilizo
katika nchi ziilizoendelea kisoka zinavyofanya.
Kwa hili Wanayanga mmtesha sana, na si dhambi klabu nyingine
kuiga haya ili kuzidi kukuza thamani ya ligi yetu.
Mchakato shirikishi, wa wazi hauna makandokando kama waleee
ReplyDeleteUkweli unaumaga.
DeleteKweli mke anampenda mumewe, huntolea mfano kwa mumewe
DeleteWalee! Baba zako eeh
ReplyDelete