June 12, 2021


 BAADA ya kwenda DR Congo na kumsainisha 
beki wa kulia wa AS Vita, Shabani Djuma, Injinia Hersi Said, amepaa na kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo imebainika kuwa anaenda kukamilisha usajili wa mshambuliaji anayekipiga katika ligi kuu nchini humo.


Hersi ambaye ni Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Jumatano alikwea pipa kwenda nchini Congo ambako alikamilisha usajili wa beki wa kulia Shabani Djuma kisha Alhamisi akapaa kuelekea nchini Afrika Kusini kukamilisha usajili wa mshambuliaji mwingine.


Chanzo chetu cha ndani kutoka nchini DR Congo kimeliambia Championi Ijumaa, kuwa ni kweli bosi wa Yanga alikutana na uongozi wa mchezaji Shabani Djuma katika hoteli ya kishua inayofahamika kwa jina la Fleuve Congo.

 Hotel hiyo inayopatikana jijini Kinshasa nchini DR Congo ambapo bosi huyo baada ya kumalizana na Djuma, Alhamisi aliaga kuwa anakwenda Afrika Kusini kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine.

“Ni kweli kiongozi wa Yanga Jumatano usiku alionekana katika hoteli inayoitwa Fleuve Congo iliyopo jijini Kinshasa ambapo walikutana na uongozi wa Shabani Djuma na bosi huyo ambapo walikuwa wakikamilisha usajili wa mchezaji huyo,” kilisema chanzo hicho.



Naye kwa upande wa meneja wa mchezaji huyo, Faustino Mukandila, alisema kuwa: “Ni kweli tumemalizana tayari na Yanga juu ya usajili wa Shaban Djuma, hivyo taratibu zilizopo kwa sasa ni kusubiri tu maandalizi ya msimu mpya kwa Yanga yaanze kisha Djuma aende Tanzania.”


Kwa upande wa nahodha mwenzake wa AS Vita Jeremy Mumbere alisema: “Djuma ameniambia kuwa tayari amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Yanga na anachosubiri ni maandalizi ya msimu mpya na Yanga kisha afanye taratibu za kuja Tanzania.”

Hersi aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiwa na Waziri wa Michezo wa DR Congo, Serge Konde na kuandika: “Ulikuwa wakati mzuri pamoja Mh. SERGE KONDE (Waziri wa MICHEZO - DR CONGO). Nikiripoti kutoka hapa KINSHASA ni mimi Eng. DJUMA HERSI SHABANI wa @yangasc.”

5 COMMENTS:

  1. Keleke na majisufu ni yaleyale nwaka jana na matokeo yake tumeyaona na yanaendelea kututesa

    ReplyDelete
  2. Umesikia ndo viongoz wa yanga wameandika hivyo

    ReplyDelete
  3. Duh kimeumana kweli kama hivyo,.,.!

    ReplyDelete
  4. Watu wanaenda congo na afrika kusini kwa biashara zao huku wakizuga wanafuata wachezaji, subirini matokeo

    ReplyDelete
  5. Wazee wa misifa, wanataka wabebwe Tena na mashabiki wa Utopolo kwakwenda kuwasajilia magalasa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic