June 30, 2021


 KLABU ya Yanga, imetenga kitita cha Sh bilioni 8.1 ili kuhakikisha msimu ujao timu yao inafanya vizuri kwenye michuano watakayoshiriki ikiwemo michuano ya kimataifa inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

 

Yanga msimu ujao inatarajiwa kushiriki Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na michuano ya kimataifa kati ya Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Bajeti hiyo imetangazwa, Jumapili na kupitishwa na wanachama wa klabu hiyo katika mkutano wao mkuu uliofanyika kwenye Ukumbi wa DYCCC, Chang’ombe, Dar es Salaam.


Katika bajeti hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, kiasi hicho cha fedha kitatumika kwa ajili ya mishahara ya wachezaji ambacho ni Sh bilioni 4.9.


Msolla alisema Sh milioni 854.7 zimetengwa kwa ajili ya bonasi kwa wachezaji wao lengo ni kuwaongezea morali ya kupambana ndani ya uwanja ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ya ushindi.Aliongeza kuwa, klabu hiyo itakusanya fedha hizo kutoka kwenye udhamini, jezi, mechi, mitandao ya kijamii na ada za uanachama.

 

“Ili timu ifanye vizuri ni lazima wachezaji na makocha wetu wapate huduma nzuri za uhakika zitakazofanya wapambane ndani ya uwanja ili tupate matokeo mazuri.

 

“Hivyo ni lazima tuwe na bajeti nzuri katika msimu ujao ili wachezaji wawe na uhakika wa kupata mishahara na bonasi kwa wakati.


“Hivyo tumetenga bajeti ya Sh bilioni 8.1 kwa ajili ya msimu ujao na fedha hizo tutazipata kwa kupitia udhamini, mauzo ya jezi, mapato ya mlangoni na mitandao yetu ya kijamii,” alisema Msolla.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic