MICHUANO ya Euro 2020 inazidi kupamba
moto barani ulaya ambapo sasa ipo katika hatua ya robo fainali, tayari
wachezaji mbalimbali wamefanikiwa kuandika rekodi zao katika michuano hiyo,
lakini hii hapa ni orodha ya mastaa waliokimbiza zaidi kwa timu nane zilizoingia
robo fainali;
Ubelgiji
Romelu Lukaku. Straika wa klabu
ya Inter Milan amekuwa katika kiweango bora ndani ya michuano hii. Ameonyesha wastani
mzuri wa matumizi ya nguvu na utulivu wake mbele ya lango umekuwa ukiwapa
wakati mgumu walinzi wanaopambana naye. Mpaka sasa amefunga mabao matatu hivyo
kujiweka katika nafasi nzuri ya kuibuka na kiatu cha ufungaji bora.
Italy
Jorginho. Huyu ni kiiungo wa
klabu ya Chelsea ambaye mara kadhaa amejikuta akikosolewa sana uchezaji wake,
ameisaidia sana Italy kupata uwiano mzuri katika eneo la kiungo.
Jamhuri ya Czech
Schick. Nyota wa kikosi cha Bayer
Leverkusen mwenye miaka 25 ambaye amefanikiwa kuonyesha uwezo mkubwa wa kufunga
kwenye michuano hii, Schick pia amekuwa kiunganishi kizuri katika mfumo wa
uchezaji wa timu ya Taifa ya Czech.
Denmark
Kinda Mikkel Damsgaard mwenye
umri wa miaka 20 anayekipiga kama kiungo ndani ya kikosi cha Sampdoria. Bila
shaka watu wengi walikuwa hawamfahamu kabla ya michuano hii ya Euro.
Lakini amekuwa nyota aliyewaka
kiasi cha kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuziba pengo la kiungo, Christian Eriksen.
Mpaka sasa Damsgaard pia amefanikiwa kufunga miongoni mwa mabao bora kwenye
michuano hii, katyika mchezo wao dhidi ya Russia.
Ukraine
Andriy Yarmolenko. Huyu ni winga
wa kikosi cha West Ham ambaye amekuwa mara kwa mara akisumbuliwa na majeraha. Ndani
ya kikosi cha Ukraine huyu ndiye amekuwa mchezaji muhimu zaidi hasa anapokuwa
kwenye robo ya mwisho ya uwanja.
Kwa sasa anakamatia nafasi ya
pili kwenye msimamo wa wafungaji bora wa muda wote kwenye kikosi cha Ukraine
akiwa ameweka kambani mabao 42.
England
Sterling ni kama vile amelipa
heshima aliyopewa na kocha wa England Southgate, hii ni baada ya kufanikiwa
kuiongoza vyema England akifunga mabao matatu mpaka sasa, Kwa sasa ni miongoni
mwa wachezaji hatari zaidi wa England.
Hispania
Pedri, Kwa sasa ana miaka 18 tu,
hiki ni miongoni mwa vipaji bora zaidi kwa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa
ya Hispania katia siku za usoni.
Amefanikiwa kucheza dakika zote
katika michezo minne ambayo Hispania wamecheza mpaka sasa.
Switzealand
Breel Embolo. Huyu ni mwanamichezo
wa kweli, akiwa na miaka 24 tayari nyota huyu amekuwa akizivutia klabu
mbalimbali ambazo zinatarajiwa kutuma ofa zao kwa klabu ya Borussia
Monchengladbach inayommiliki. Amefunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Wales.







0 COMMENTS:
Post a Comment