July 2, 2021


 NAHODHA wa kikosi cha Azam FC, Agrey Morris amesema kuwa watapambana kufanya vema katika mechi zao ambazo zimebaki.

Ikiwa ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 64.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya Simba ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex 14.

Morris alikuwa kwenye kikosi cha kwanza kilichopoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba ila ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho.

Nyota huyo mzawa amesema:"Ni kweli ushindani ni mkubwa kwenye ligi hilo tunalijua lakini nasi tuna kazi kubwa ya kufanya vizuri.

"Kikubwa mashabiki watupe sapoti kwenye mechi ambazo zimebaki tunaamini tutafanya vizuri," .    

4 COMMENTS:

  1. Mpambane nini nyinyi tawi LA Simba? Labda mngekuwa mnacheza na Yanga ndio mngetoa mimacho

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aibu gani hii jamani! Tangu lini Azam akawa tawi la Simba? Kuwa na aibu japo kidogo ndugu

      Delete
    2. Azam ni tawi letu sisi Yanga. Usiogope kuweka wazi. Kocha wao alikuwa wetu. Na wachezaji kibao ni vibaraka wetu na nakupa mfano mmoj tu SURE BOY

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic