July 17, 2021


HAJI Mpili, maarufu kama Mzee Mpili ambaye ni mwanachama wa Klab ya Yanga amesema kuwa laiti kama mchezaji Bernard Morrison angekuwa ndani Yanga angafanya vizuri zaidi tofauti na sasa.

Morrison amekuwa kwenye mvutano mkubwa na Yanga ishu ya mkataba wake ambapo Yanga wamekuwa wakidai kwamba ana dili la miaka miwili na mchezaji anadai kwamba dili lake lilikuwa ni la miezi sita lilikwisha.

Kuhusu hilo ambapo Yanga wameeleza kuwa kesi yake ipo kwenye ahakama ya usuluhishi, (Cas) Mzee Mpili amebainisha kuwa kesi hiyo ni nzito.

Mpili amesema:-“Akili yake waliivuruga na mimi naamini kama angekuwepo Yanga basi angefanya vizuri sana tofauti na sasa, kwa sababu wanasema hayupo kwenye timu ameondoka.

 


“Ndio maana tumepeleka CAS na kesi yake ni nzito na Morisson mwenyewe alitaka kesi yake iamuliwe hapa na mpira wake umeshapotea.


“Tarehe tatu alionyesha kama shoo tu hakufanya chochote kwani tulizuia mpira wake, na kwenye simu yangu sina namba ya Morisson na siwezi kuongea nae.

 

“Mzee Dalali amesema anatangulia kigoma na anaenda kunipiga lakini akumbuke kuwa na Haji Manara alisema hivo hivo kuwa atanipiga tatu kwenye mchezo uliopita na nilimpiga na hela katoa, sahizi sio bao moja itakuwa zaidi ya kuhesabu.

 

“Sisi hatuwezi kubadilisha uwanja ni ule ule pale pale kigoma sisi mipango ya kucheza mpira tumeshamaliza na watu wangu wameshafika.


"Simba wana kikosi kizuri lakini mimi na wachezaji wangu wa kuokota okota nitawapiga hivo," .



13 COMMENTS:

  1. Hahaaa, huyu mzee kanogewa na pesa ya wanasimba. Kigoma atapigwa, mzee Mpili bora asiende kabisa.

    ReplyDelete
  2. Hizi habari za hiki kigagula mnapenda kuzipublish za nini? Kama yeye kamroga Morisson, sawa aendelee mbele, kelele za nini? Anataka kuwaaminisha watu kuwa sasa yanga inashinda kwa sababu yeye ndio anacheza na sio wachezaji, ovyo kabisa.

    ReplyDelete
  3. Mzee ajiangalie hasiichukulie Simba kiboya ajue hiyo ni fainali Simba anajulikana ktk fainal stage yukoje na mechi hiyo inashikiria hatma ya benchi la ufundi na baadhi ya wachezaji wa Simba. Kocha Gomes anatakiwa aonyeshe ubora hapo maana akifungwa na hapo hata ngao ya jamii na kwenye ligi msimu hujao tukiendelea kuwa naye tutafungwa na yanga na team zinazocheza vurugu vurugu Kama yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tulizeni mishono Mzee Mpili endelea na tambo zako asikutishe nyang'au yeyote. Kazi iendelee

      Delete
  4. Daah kizee kinatangaza ndumba live kbs,

    ReplyDelete
  5. Viongozi Yanga mzuieni huyu mzee. Hivi sasa kila mtu anajua kuwa ushindi wetu ni matokeo ya ushirikina. Hata kama sisi hatuna mpira lakini huyu mzee anatupakazia vibaya. Mbona zamani tulikuwa hatusikii? Kwani tulikuwa hatutimii mazingara? Haya mambo yalifanywa siri
    Msipomzuia basi hadi mipango ya kuhonga marefa itafichuka

    ReplyDelete
  6. Mchawi anamhofia mchawi mwenzie kama ww si mchawi kwann uhofie wote ni washirikina endeleeni kumhofia mshirikina mwenzangu

    ReplyDelete
  7. Mzee anamaliza umri wake na mikwara mingi natamani kumuona akiwa kachezea kichapo cha mbwa mwizi ili tuone atakuja na mashairi gani kikubwa tumuombee uhai ili ayashuhudie yaliyomkuta mzee mzimba Akilimali na wazee wengine wa utopolon

    ReplyDelete
  8. Mzee Mpili kuna mbwa koko wanaweweseka huku, chapa kazi kama inawauma wachomoe waende zao. Yanga bhana, Kigoma kawapige kwenye mshono palepale

    ReplyDelete
  9. Replies
    1. Kama wazee wa mapaka tu hakuna tofauti. Tofauti ni kilio na kubwatuka tu baada ya kusakafiwa Kwa Mkapa

      Delete
  10. Yanga kama nyoka kifutu sumu yake

    ReplyDelete
  11. Hela ya Mnara imemteguwa akili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic