July 16, 2021

AMEMALIZA kibabe ndivyo unavyoweza kusema, hii ni baada ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima kuhitimisha maisha yake ya soka ndani ya klabu ya Yanga huku akiwa amefanikiwa kutwaa makombe 11 kwenye ardhi ya Tanzania.

Niyonzima aliagwa rasmi na mashabiki na wapenzi wa Yanga jana Alhamisi kupitia mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu, uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salam. Niyonzima alijiunga na Yanga akitokea ndani ya kikosi cha klabu ya Rayon Sports ya Rwanda mwaka 2011.

nyota huyo ameichezea Yanga katika vipindi viwili tofauti kuanzia mwaka 2011 mpaka 2017, na baada ya hapo alijiunga na Simba aliyoichezea mpaka mwaka 2019. Januari 2020 Niyonzima alijiunga na Yanga kwa kipindi cha pili ambapo anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Kwa kipindi chote alichocheza soka ndani ya ardhi ya Tanzania Niyonzima amefanikiwa kutwaa makombe matano ya Ligi Kuu Bara, makombe matatu ya ngao ya jamii, kombe moja la CECAFA Kagame, Kombe moja la FA na kombe moja la Mapinduzi.

 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic