July 8, 2021

BAADA ya Yanga kukamilisha usajili wa aliyekuwa  beki wa kulia wa AS Vita, Shaban Djuma, mmiliki wa nafasi hiyo kwa sasa, Kibwana Shomari ameufungukia usajili wa beki huyo huku akimkaribisha ndani ya klabu hiyo.

Kibwana Shomari na Shabani Djuma wote wanacheza katika nafasi moja ya beki wa kulia, hivyo wataungana na beki mwingine Paul Godfrey Boxer katika kuwania namba chini ya kocha Nassredine Nabi.

Akizungumzia usajili huo Kibwana amesema kuwa  ujio wa Shabani Djuma ndani ya Yanga sio swala geni kwenye mpira, kwani ili timu iweze kuwa bora basi huitaji kuwa na wachezaji bora kwa manufaa ya timu ili iweze kufikia malengo yake hivyo yeye anamkaribika mchezaji huyo ndani ya Yanga 

“Suala la Yanga kusajili beki mwingine wa kulia sio swala geni kwenye mpira, hivyo mtu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine  kama ilivyotokea kwa Djuma ni vitu vya kawaida na mpira ndio ulivyo hata sisi hatukuwa hapa lakini leo tupo Yanga .

“Ni faida kwa Yanga kuwa na wachezaji bora ambao wataisaidia timu kufanya vizuri, hivyo muhimu ni kutimiza majukumu ambayo mwalimu anatupatia wachezaji kwa ajili ya kufikia malengo yetu,kama ni kweli amesajiliwa na Yanga tunamkaribisha,” amefunguka Kibwana. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic