July 7, 2021


 HUENDA nyota wa kikosi cha Azam FC, David Kissu msimu ujao akaondolewa kwenye kikosi hicho kwa kuwa hayupo kwenye mpango wa Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Taarifa zimeeleza kuwa Kissu ambaye ni ingizo jipya ndani ya Azam FC ambapo aliibuka huko akitokea Klabu ya Gor Mahia ya Kenya alikuwa akicheza na Dickson Ambundo ambaye naye ni mzawa na kwa sasa anakipiga ndani ya Dodoma Jiji.

Alianza kwa kasi msimu huu ambapo alikuwa chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba ambaye alichimbishwa kutokana na kile ambacho kilielezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo.


"Kissu anaweza kuondoka ndani ya Azam FC msimu ujao kutokana na kutokuwa na nafasi hivyo ni suala la kusubiri na kuona namna gani maisha yatakuwa msimu ujao," ilieleza taarifa hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin hivi karibuni alisema kuwa masuala ya ufundi yapo kwenye benchi la ufundi," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic