CHARLES Zulu, kiungo mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa amekuja kwa ajili ya kuchukua mataji ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.
Raia huyo wa Zambia alisaini dili la miaka miwili Julai 4 akitokea Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini ikiwa ni ingizo jipya ndani ya timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex.
Nyota huyo amesema:"Nina furaha kuwa ndani ya Azam FC kwa kuwa ni moja ya timu bora ninajivunia kwa hilo hasa baada ya kuweza kusaini hapa.
"Nimekuja hapa kushinda mataji, nataka kufunga mabao, kutoa pasi za mabao, kwa sababu hiyo ndio kazi yangu ambayo imenifanya niweze kuja hapa," amesema.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Azam FC ipo nafasi ya tatu na ina jumla ya pointi 64 baada ya kucheza jumla ya mechi 32.
Haha mataji gani tena? Maana azam inakuwa bora sana lkn mwisho wa siku inaambulia nafasi ya tatu
ReplyDeleteKama ana mkataba wa zaidi ya miaka 5 , maana Kuna litimu moja Lina kauli mbiu ya kuichukua ubingwa back to back for ten years na Sasa imebaki miaka 5
ReplyDelete🤣😂😅 mataji ya umisi labda
ReplyDeleteHahahaha ajipange vema maana ligi ya bongo sio lelemama watu wanakimbizana na Muda vema kama kaja kwa mataji me yanga ila tunatamani kuona ligi bora yenye ushindani sio Yanga na simba tu
ReplyDelete