UONGOZI wa KMC umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wana asilimia kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.
"Sisi kama Kinoboys hatuwaogopi ila tunawaheshimu kwa sababu tunakwenda kucheza mchezo ambao tulikuwa tunajua kwamba tunakwenda kucheza tarehe 7.
"Kila mchezaji yupo tayari hivyo mashabiki ninaowamba kesho wajitokeze kwa wingi na jezi za KMC kwa kuwa tupo tayari na tutatoa burudani.
"Niwahakikishie mashabiki kwamba kesho waje uwanjani na waamini kwamba tunachukua pointi tatu kwa kuwa tutatoa burudani na vitu ambavyo wataviona ni vile ambavyo hawajawahi kuona kwenye mechi zetu za nyuma," amesema.
Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 1-0 KMC hivyo unatarajiwa kuwa mchezo wa kisasi.
Simba inapambana kusaka pointi tatu ili kutwaa ubingwa wa ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake ni 73 huku KMC ikiwa nafasi ya 6 na pointi zake ni 42.
Nyie ni tawi la simba
ReplyDeleteKMC haijawahi kuwa tawi la Simba hata siku moja tena ktk timu zinazo ikazia Simba yenyewe inaongoza ikifuatiwa na Utopolo
ReplyDeleteUbishi wa nini, ngoja 4 zinasubiri
Delete