July 12, 2021


 HABIB Kondo, Kocha Msaidizi wa KMC amesema kuwa kwa namna ambavyo wamejipanga katika mechi zao mbili zilizobaki hawatakubali kudondosha pointi tena.

Baada ya kucheza jumla ya mechi 32 imebakiza mechi mbili ambazo ni dk 180 zenye pointi sita. Kwenye msimamo ipo nafasi ya 6 na pointi zake ni 42.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kondo amesema kuwa kupoteza mbele ya Simba kumewapunguzia kasi yao ya kufikia malengo lakini hawajakata tamaa ya kuendelea kupambana.

Kondo amesema:-“Ukitazama mchezo wetu uliopita tulijifelisha sisi wenyewe hapo hatuna cha kumlaumu. Kwa kuwa tuna mechi mbili ambazo zimebaki hizo tutapambana ili kupata pointi tatu na inawezekana.

“Kwa namna ambavyo tumejipanga uhakika ni mkubwa kushinda kwani makosa ambayo tumeyafanya tunakwenda kuyafanyia kazi na inawezekana kupata pointi tatu kwa uhakika licha ya kwamba ushindani ni mkubwa,” amesema Kondo.

Ni mechi mbili ambazo zimebaki mikononi mwa KMC ni dhidi ya JKT Tanzania itakuwa Julai 14 na Ihefu Julai 18.

Mchezo wake uliopita kwenye ligi iliyeyusha pointi tatu mazima mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 2-0 jambo ambalo limefanya timu hiyo kupoteza pointi sita mbele ya mabingwa hao wa ligi.

Mzunguko wa kwanza walifungwa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa hivyo ndani ya dk 189, KMC imefungwa mabao matatu na kuacha pointi sita mazima mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic