July 12, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utasepa na pointi sita zote ambazo wanazipambania kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara ili kutimiza malengo yao ambayo wamejiwekea.

Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imekusanya pointi 70 baada ya kucheza mechi 32, imebakiza mechi mbili zenye pointi sita ni mbele ya Ihefu FC na Dodoma Jiji.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa namna ambavyo wamejipanga wana uhakika wa kusepa na pointi zote sita ambazo wanazipambania.

“Nikuhakikishie kwamba mechi zetu mbili ambazo zimebaki hapo tuna uhakika wa kuchukua pointi zote sita hii yote inatokana na maandalizi mazuri ambayo tumefanya.

“Kikubwa ni kuona kwamba kwenye kila mechi tunafanya vizuri na hilo lipo wazi ukizingatia kwamba kila mchezaji anatimiza majukumu yake anayopewa,” amesema Bumbuli.


Ikiwa Yanga itasepa na pointi zote sita itafanya ifikishe jumla ya pointi 76 kwa kuwa sasa ina pointi 70 baada ya kucheza mechi 32.

Bingwa ni Simba mwenye pointi 79 ametangazwa jana akiwa na mechi mbili mkononi kwa sababu pointi ambazo amezifikia kwa sasa haziwezi kufikiwa na timu yoyote ndani ya Bongo.

7 COMMENTS:

  1. Atuambie sasa bado wamo kwenye mbio za ubingwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bado hamjamwelewa Bumbuli mpaka sasa?

      Delete
  2. Wameukosa ubingwa na iliobaki waendelee na porojo lisilo na mwisho

    ReplyDelete
  3. Simba wasisajiri wakaa benchi au wenye majeraha na wasituletee wachezaji wa majaribio Kama wanataka kuendeleza history nzuri na kufika mbali

    ReplyDelete
  4. Wameanza kujielewa now congratulations

    ReplyDelete
  5. Alisema mpaka tarehe 23 July itakuwa imejulikana Kama yanga ndo bingwa hivyo tusubiri mpaka tr 23 July yanga watangaze ubingwa teeeteee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic