July 7, 2021

 LUIS Suarez nyota wa kikosi cha Atletico Madrid ambao ni mabingwa wa La Liga ni mzee wa kutupia ambapo mpaka msimu wa 2020/21 amecheza jumla ya mechi 654 katika mashindano yote. 

Rekodi zinaonyesha kwamba ametupia jumla ya mabao 424 na kutoa pasi za mwisho 238.

Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay aliwahi kucheza Ligi Kuu England ndani ya Liverpool inayonolewa na Kocha Mkuu Jurgen Klopp msimu wa 2011/14 alicheza jumla ya mechi 110 na kutupia mabao 69.

Aliibuka ndani ya Atletico Madrid msimu wa 2020 bure baada ya mabosi wa Barcelona kumpa mkono wa kwa heri ambapo aliibuka hapo msimu wa 2014 mpaka msimu wa 2020 alikuwa amecheza jumla ya mechi 191 na alitupia mabao 147.

Kwa sasa ndani ya Atletico Madrid nyota huyo mwenye miaka 34 amecheza jumla ya mechi 32 na kutupia mabao 21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic