July 17, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Barcelona, Lionel Messi yupo kwenye hatua nzuri ya kuongeza dili jipya ndani ya timu yake hiyo ambayo anaitumikia na amekubali kupunguza mshahara wake.

Nyota huyo ambaye ametoka kutwaa taji la Copa America baada ya timu yake ya taifa ya Argentina kushinda bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Brazil kwenye mchezo wa fainali, Uwanja wa Maracana, ambapo bao la ushindi lilifungwa na Angel di Maria ambaye ni kiungo anayekipiga ndani ya PSG.

Kwa sasa nyota huyo anajiandaa kusaini dili la miaka mitano kwa ajili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo inayoshiriki La Liga, Hispania baada ya dili lake la awali kumeguka.

Mbali na kukubali kusaini dili hilo, Messi mwenye miaka 34 amekubali kukatwa mshahara kwa asilimia 50 kutokana na hali ngumu inayopitia timu hiyo kwa wakati huu kutokana na kuyumba kulikosasbabishwa na janga la Corona.

Kwa mujibu wa gazeti la ESPN, limesema kuwa mshambuliaji huyo amekubali kusaini dili jipya na kuwapiga chini Manchester United na PSG ambao walikuwa wanatajwa kuiwania saini yake.

1 COMMENTS:

  1. Huyu mchezaji ni mzuri ila hajiamini Hana CV za kutosha yaani unacheza team moja tu tutakuhitaje mchezaji wa dunia wakati hujawahi kuchukua kombe la dunia uikiwa na nchi yako ukicheza pia umekaa klabu moja tu au ligi moja tu ya laliga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic