MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Azam FC, Prince Dube anatarajiwa kuukosa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa sababu, Azam FC inapambana kuweza kutimiza lengo la kumaliza nafasi ya pili huku Simba ikihitaji kupata ushindi.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 64 ili iweze kumaliza katika nafasi ya pili inapaswa kushinda mechi zote kwa mabao mengi zaidi huku ikisubiri matokeo ya Yanga ikiwa itapoteza mechi zake zote mbili jambo ambalo ni gumu kutokea lakini kwenye mpira jambo lolote linawezekana.
Yanga ipo nafasi ya pili na ina mechi mbili mkononi ikiwa na pointi 70 kwa upande wa mabao Yanga imefunga mabao 50 huku Azam FC ikiwa imefunga mabao 48.
Dube kwenye mabao 48 amehusika katika mabao 19, akiwa amefunga mabao 14 na kutoa pasi tano za mabao.
Nyota huyo alikosa mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali mbele ya Simba kwa kufungwa bao 1-0 na Dube alikuwa jukwaani akitazama mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya tumbo ambayo yamekuwa yakijirudiarudia.
0 COMMENTS:
Post a Comment