July 12, 2021


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mechi zao zilizobaki ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga wataendeleza kuchukua ushindi kwa kuwa ni malengo yao waliyojiwekea.

Simba ikiwa imekusanya jumla ya pointi 79 ipo nafasi ya kwanza na imebakiza mechi mbili za ligi kwa kuwa imecheza jumla ya mechi 31 msimu wa 2020/21.

Akizungumza na Saleh Jembe, Gomes amesema kuwa ushindi wao mbele ya Coastal Union umewarejesha kwenye reli kwa kuwa kasi ilirejea baada ya ushindi wao mbele ya KMC.

Pia wana kazi ya kucheza na watani zao wa jadi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho itakuwa ni Julai 25 watakapokutana na Yanga.

“Hatujawa kwenye furaha kubwa hasa ukizingatia tumetoka kupoteza mbele ya Yanga ila ni suala la matokeo. Ambacho kimebaki kwa sasa ni kuona kwamba mechi zetu zote kuanzia hizi za ligi mpaka ile ya fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga tunashinda.

“Tulibainisha tangu awali kwamba tunahitaji kushinda mechi zote, kushinda mataji yote hivyo jambo pekee ambalo tunalo kwa sasa ni kuendelea kushinda kwenye mechi zetu zote.

"Kupoteza mchezo uliopita haina maana kwamba hatuna ubora hapana lakini tuna kazi ya kufanya na mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Gomes.  

Mechi za Simba itakuwa ni dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex, Julai 14 na Namungo FC, Julai 18, Uwanja wa Mkapa.

2 COMMENTS:

  1. Azam complex ina uwezo wa kihimili mechi kubwa kama hii?

    ReplyDelete
  2. walicheza na Yanga hapo hapo Azam Complex

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic