July 6, 2021


 MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Mzee Hassan Dalali amesema kuwa kwa sasa hakuna haja ya kumtafuta mchawi baada ya timu hiyo kupoteza kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mzee Dalali alisema kuwa walikuwa wanahitaji kushinda kwenye mchezo huo lakini kwa kuwa ilikuwa tofauti hakuna haja ya kumtafuta mchawi.


“Kilichotokea Julai 3 ni matokeo tu ya mpira, lazima tukubali licha ya kwamba inaumiza. Tujipange kwa ajili ya mechi nyingine tusianze kumtafuta mchawi nani kwa kuwa hiyo itaturudisha nyuma.


“Nilikwambia kwamba mpira wa Simba na Yanga hauna ufundi, hilo lilijitokeza. Kikubwa viongozi wajipange, Wanachama tuendeleze umoja tushikamane nina amini kwamba makosa ambayo yametokea benchi la ufundi litafanyia kazi.


“Wanachama tutulie, tuache mihemuko tuanze kucheza kwanza tutetee ubingwa wetu kwenye michezo. Lawama kwa wachezaji tuache haya ni mambo ya kawaida inaumiza sana ila tumefungwa, hatuwezi kufanya jambo jingine, matokeo yale kila mmoja amekuwa na maneno kikubwa tushikiriane,” alisema Dalali.

2 COMMENTS:

  1. Kwel kabisa mzee,umeongea point nzuri mno,tukae chin tujitafakari wapi tulikwama,Halafu tukikutana Kigoma,

    ReplyDelete
  2. Hizi ndo kauli za kisoka sasa! Cyo zile za mzee mpili kujinadi kuwa yy ndo aliyekuwa mchezaji namba 1 juzi j1! ,,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic