July 6, 2021


 KIUNGO mshambuliaji mpya wa kikosi cha Manchester United, Jadon Sancho amesema kuwa kwa sasa hataki kuzungumzia jambo lolote kuhusu timu hiyo.

Sancho raia wa England alicheza mchezo wa Euro 2020 dhidi ya Ukraine na timu yake iliweza kushinda mabao 4-0 na kuweza kutinga hatua ya nusu fainali.

Tayari nyota huyo amesajiliwa na United kwa dau la pauni milioni 73 hivyo msimu ujao atakuwa ndani ya Old Trafford.

Alipoulizwa kuhusu Manchester United nyota huyo alisema:"Kwa sasa sitaki kuzungumzia kuhusu Manchester United, nafahamu kwamba nipo kwenye timu ya taifa na natakiwa kuzungumzia kuhusu timu ya taifa," .

Leo Julai 6 inatarajiwa kuchezwa nusu fainali huku timu ya taifa ya England ikitarajiwa kucheza kesho Julai 7 dhidi ya Denmark na ya kwanza itakuwa kati ya Italia dhidi ya Hispania ambayo itachezwa leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic