July 1, 2021


 KUELEKEA kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Simba v Yanga, Julai 3, guu la kulia la nyota wa Yanga Said Ntibanzokiza,’Saido’ ni la kuchungwa na wapinzani wake Simba  kwa kuwa limekuwa na nguvu kila awapo uwanjani.

Akiwa amehusika katika jumla ya mabao 9 kati ya 49 yaliyofungwa na timu hiyo ni mabao manne amefunga na kutoa pasi tano za mabao. Ni kwa mguu wa kulia amefunga mabao manne na kutoa pasi tatu huku akitumia mguu wa kushoto kutoa pasi mbili za mabao.

Wakati Simba wakichunga guu la kulia, kwa Luis Miquissone Yanga wanakazi ya kuchunga guu la kushoto ambapo katika mabao 9 ambayo amefunga ni mabao 7 alitumia guu la kushoto, bao moja kwa kichwa na moja kwa guu la kulia.


Kwa Saido ilikuwa namna hii kwa guu la kulia dk 69 alipachika bao la kwanza na alitoa pasi ya kwanza dk 75 ilikuwa ni kwa guu la kulia, mbele ya Dodoma Jiji, Desemba 19, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Alimtungua Jeremiah Kisubi dk 76 ilikuwa Uwanja wa Nelson Mandela, Desemba 31,mbele ya Prisons, kwa guu la kulia.


Pasi nyingine alitoa dk 46 mbele ya KMC, Aprili 10, Uwanja wa Mkapa kwa guu la kulia. Alimtungua kipa wa Gwambina FC, Aprili 20, Uwanja wa Mkapa dk 90+4 kwa guu la kulia.



Alitoa pasi ya bao Juni 20 mbele ya Mwadui kwa guu la kulia dk 21 Uwanja wa Mkapa. Bao moja alimtungua kipa wa Ruvu Shooting kwa pigo huru ilikuwa ni Juni 17, Uwanja wa Mkapa dk 79 kwa guu la kulia.


Kwa guu la kushoto ilikuwa mbele ya Ihefu alitoa jumla ya pasi mbili, dk 12 na 49 ilikuwa Desemba 23 mbele ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine ni kwa guu la kushoto.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic