KIKOSI cha Polisi Tanzania leo Julai 20 kimetangaza rasmi kuachana na nyota wake 13 ambao hawatakuwa katika kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.
Nyota hao baadhi yao walikuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Malale Hamsini ikiwa ni pamoja na kiungo Hassan Nassoro na mshambuliaji wake Kaheza.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Polisi Tanzania imesema kuwa inawashukuru wachezaji hao kwa mchango wao na kwa namna ambavyo walikuwa nao.
Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kandarasi zao kufika ukomo na hawakuwa tayari kuwaongezea huku wakiwaombea kila la kheri huko ambapo watakuwa.
Wachezaji hao ni:-
Marcel Kaheza, Mohamed Bakari,Mohamed Yusuph, Mohamed Kassim, Ramadhan Kapele,Pato Ngonyani,Pius Buswita, Jimmy Shoji,Joseph Kimwaga,George Mpole,Emmanuel Manyanda,Erick Msagati na Hassan Nassoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment